Wednesday, December 25, 2024
spot_img

POLISI TANGA WASAKA FAILI LA MGOGORO WA KSIJ TANGA JAMAAT, WAONYA HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA

RIPOTA PANORAMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linafuatilia faili la mgogoro unaofukuta katika KSIJ Tanga Jamaat unaodaiwa kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Henry Mwaibambe amesema faili hilo halijafika mezani kwake lakini amemuagiza Kamanda wa Makosa wa Jinai wa Mkoa wa Tanga (RCO) aliyesema naye ni mgeni katika ofisi hiyo kulisaka faili hilo na kulifanyia kazi kikamilifu.

Kamanda Mwaibambe ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa kuhusu madai ya kuwepo tishio la uvunjifu wa amani katika KSIJ Tanga Jamaat ambao chanzo chake kinadaiwa kuwa ubadhilifu wa fedha wa vitisho.

Awali, Tanzania PANORAMA Blog ilidokezwa na vyanzo vya habari kutoka ndani ya KSIJ Tanga Jamaat kuwa mwenyekiti wa Jamaat hiyo, Hussein Walje anadhulumu fedha za walemavu na wajane, amepoka uongozi wa Jamaat ambayo sasa anaiongoza kiimla na kwamba yeye na mpambe wake anayedaiwa kuwa na ukwasi mkubwa wanatishia kuwapoteza wanaohoji ubadhilifu wa fedha na kupinga uongozi wa kiimla ndani ya Jamaat hiyo.

Inadaiwa mgogoro huo ulichunguzwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga lakini kabla halijaanza kuchukua hatua, lilipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa mkoa huo kusitisha utekelezaji wa hatua lililozokusudia hivyo faili hilo likawekwa kapuni.

Kamanda Mwaibambe katika majibu yake kwa Tanzania PANORAMA Blog amesema hana taarifa za kuwepo kwa faili hilo wala uchunguzi uliofanywa na polisi kuhusu mgogoro wa Jamaat hiyo na hata RCO, ambaye naye amesema ni mgeni katika ofisi hiyo hana taarifa za uwepo wa faili hilo; kabla ya kuahidi kulifukua lililopo na kulifanyia kazi.

Mwenyekiti wa KSIJ Tanga Jamaat, Hussein Walje

“Wanalitafuta hilo jalada nataka waniletee nilione. Huyu RCO aliyepo naye ni mgeni ana kama mwezi mmoja, nitakupa jibu nikishaliona lakini kama kuna mtu anatishia watu mimi nawapenda sana watu wa aina hiyo, napenda kushughulika nao. Kama anatishia watu, hakuna mtu aliyejua ya sheria. Taarifa nimepata, acha nione faili. Tutafanya kazi yetu,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Zaidi ya wanajumuiya 40 wa KSIJ Tanga Jamaat wanamtuhumu Walji kuiongoza Jamaat hiyo kiimla, kufuja mali za Jamaat na kudhulumu fedha za misaada za wajane na walemavu na sambamba naye, wanamtuhumu pia mmoja wa wafanyabiasha mwenye ukwasi mkubwa wanayemtaja kuwa mshirika wa karibu wa Walji kwa kuwatisha kuwa atawapoteza duniani na kwamba anatumia uwezo wake wa kifedha kuwabambikia kesi polisi.

Walji alipoulizwa kuhusu tuhuma anazoelekezewa hakukanusha wala kukubali na badala yake alisema mambo hayo anaweza kuyazungumzia iwapo Tanzania PANORAMA Blog itafika ofisini kwake na kukutana naye ana kwa ana.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya