Thursday, July 17, 2025
spot_img

RPC TANGA ASEMA HAUJUI MGOGORO WA TSIJ JAMAAT

RIPOTA PANORAMA

KAMANDA wa Polisi (RPC) wa Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Henry Mwaibambe amesema haujui mgogoro unaofukuta kwa muda mrefu katika Jamaat ya TSIJ ya mkoani Tanga.

Akizungumza jana na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu mgogoro huo kuibua viashiria vya kutishia amani huku polisi wakidaiwa kuwa na taarifa za malalamiko ya wanajumuiya ya kumkataa mwenyekiti wao wanayemtuhumu kutafuna fedha za misaada za wajane na walemavu, Kamanda Mwaibambe alisema hata yeye taarifa hizo amesizoma kwenye mtandao lakini hazijafika kwake.

Sambamba na Mwenyekiti Walji, mwingine anayetuhumiwa katika mgogoro huo ni mmoja wa matajiri wenye ukwasi mkubwa mkoani Tanga (jina tunalihifadhi kwa sasa) kuwa amekuwa akiwatishia maisha na kujigamba kuwa katika biashara zake yeye amekwishapoteza watu wengi hivyo haoni tabu kuendelea kupoteza wengine.

ā€œHata mimi nimesoma tu kwenye mtandao kuhusu hizo taarifa lakini mimi binafsi sijapata taarifa hizo, hapa ndiyo nataka nifuatilie, labda niulize kama walileta malalamiko lakini mimi binafsi sijalipata hilo. Unajua RPC ni ofisi labda kuna taarifa zilifika mimi nikiwa sijafika. Ngoja nifike hapo maana sasa hivi ndiyo nataka kwenye msiba kwa hiyo kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu sijajua lakini tumepokea hizo taarifa, tunazifuatilia, tunachunguza kujua ukweli, kiini cha mgogoro ni kitu gani. Nipe muda kidogo niongee na OCD,ā€ alisema Kamanda Mwaibambe.

Wakati Mwaibambe akisema hayo, baadhi ya wanajumuiya ya Jamaat ya KSIJ Tanga wanaomtuhumu Mwenyekiti wao Hussein Walji, ambao awali walieleza kuwa taarifa za mgogoro wao zimekwishafikishwa ofisini kwa RPC muda mrefu, wameendelea kusisitiza kuwa taarifa za mgogoro wao ikiwa ni pamoja na ripoti kamili ya ubadhirifu wa fedha za Jamaat unaofanywa na Walji, ziko ofisini kwa RPC.

Zaidi ya wanajumuiya 40 wa Jamaat ya KSIJ Tanga wanamtuhumu Walji kuiongoza Jamaat hiyo kiimla, kufuja mali za Jamaat na kudhulumu fedha za misaada za wajane na walemavu na sambamba naye, wanamtuhumu pia mmoja wa wafanyabiasha mwenye ukwasi mkubwa wanayemtaja kuwa mshirika wa karibu wa Walji kwa kuwatisha kuwa atawapoteza duniani na kutumia uwezo wake wa kifedha kuwabambikia kesi polisi.

Walji ambaye juzi alihojiwa na Tanzania PONORAMA Blog kuhusu tuhuma anazoelekezewa na wanajumuiya ya Jamaat ya Tanga, alishindwa kukanusha wala kukubali na badala yake alisema mambo hayo anaweza kuyazungumzia iwapo Tanzania PANORAMA Blog itafika ofisini kwake na kukutana naye ana kwa ana.

Haya yanatokea ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuunda tume ya kungalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai ambayo itafanya kazi hiyo kwa muda wa miezi minne.

Katika uzinduzi huo Rais Samia, pamoja na mambo mengine alilinyooshea kidole Jeshi la Polisi kuwa miongoni mwa taasisi zenye sifa zisizoridhisha na linalosemwa vibaya na wananchi katika utekelezaji wa majukumu yake na sambamba na Rais Samia, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango naye alilinyooshea kidole Jeshi la Polisi kwa kutotekeleza wajibu wake ipasavyo.

TANZANIA PANORAMA BLOG INAENDELEA KUFUATILIA SAKATA HILI.    

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya