Friday, April 25, 2025
spot_img

NHC MOROCCO SQUARE YAANZA KUCHANUA

RIPOTA PANORAMA

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) na Kampuni ya KingJada Hotels and ApartimentS wamesaini mkataba wa biashara ya upangaji wa jengo la hoteli lililopo kwenye moja ya majengo ya kisasa ya kibiashara yanayomilikiwa na NHC la Morocco Square.

Utiaji Saini huo ulifanyika jana katika majengo ya Morocco Square yalipo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na uongozi wa juu wa NHC na ule wa Kampuni ya KingJada Hotels and Apartiments; kampuni ambayo ina uzoefu wa uendeshaji biashara za hoteli zenye hadhi za kimataifa duniani.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu alisema uamuzi wa Kampuni ya KingJada Hotels and Apartiment kuwekeza kwenye Sekta ya Hoteli kwa kupanga jengo lenye hadhi kubwa na lililo kwenye eneo zuri la kibiashata jijini Dar es Salaam unatokana na mazingira mazuri ya uwezekaji na ufanyaji biashara yaliyowekwa na Serikali katika Sekta ya Miliki.

Mchechu alisema mradi wa Morocco Square umetoa fursa ya kukuza uchumi kupitia Kampuni ya KingJada pamoja na wale watakaotoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye mradi huo.

Alisema hivi sasa NHC imejizatiti kuibua miradi mingi ya ujenzi wa nyumba ili kuwapatia Watanzania wengi fursa za makazi na biashara na kwamba mbali na mradi huo wa Morocco Square ambao ni moja ya majengo mazuri yanayovutia na kuongeza uzuri wa taswira ya Jiji la Dar es Salaam, shirika hilo litaendelea kutekeleza miradi mingi kwa kasi.

“Fursa zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita katika Sekta ya Uwekezaji zimechangia kwa kiasi kikubwa kuwasukuma KingJada Hotels and Apartments kuwekeza katika mradi wa Morocco Square. Ninaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuliunga mkono shirika na Sekta ya Miliki nchini na kuhimiza uwekezaji ambao umekaribisha wawekezaji wengi kwa ajili ya kuwekeza na kulipatia Taifa letu mapato zaidi.

“Utekelezaji wa mradi wa Morocco Square, mbali na uwepo wa hoteli pia kuna maduka makubwa ya biashara na nyumba za makazi ambapo kwa sasa zimebakia shughuli chache ili kukamilisha mradi huu utakaoleta chachu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

“Ninaipomgeza Kampuni ya KingJada kwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye hoteli hii kwani itafanya biashara nzuri kwa kuwa eneo la Morocco liko sehemu nzuri inayofikika kwa urahisi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na pia uwepo wa hoteli hii utakuwa ni chachu ya ukuaji wa biashara zingine katika majengo ya Morocco Sqaure,” alisema Mchechu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu akikabidhiana mikataba ya upangaji wa hoteli kwenye majengo ya Morocco Square na Mkurugenzi wa Kampuni ya KingJada Hotels and Apartiments, Sanjay Shah muda mfupi baada ya utiaji saini mikataba hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Szlaam.

Aidha Mchechu alisema NHC inajenga majengo lakini dhamira yake inatimia baada ya majengo yanayojengwa kupata wanunuzi na wawekezaji na pia kuanza kupatikanaji kwa wawekezaji kunasaidia shirika kutimiza azma yake ya kuchangia uboreshaji wa uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya KingJada Hotels and Apartments, Risasi Mwaulanga alisema kampuni yake ina imani NHC itafika mbali kimalengo na kimikakati; mambo ambayo yatawasaidia wawekezaji kufikia malengo yao ya kibiashara.

“Uzoefu wa kampuni yetu katika Sekta ya Hoteli nchini India pamoja na uendeshaji wa hoteli za nyota tano ndani na nje ya nchi ya India umetuonyesha kuwa ubia huu utaleta tija kubwa kwa NHC na kwamba mafanikio ya Hoteli ya KingJada yatakuwa chachu ya ukuaji wa biashara zingine katika jengo la Morroco Square,”.alisema Mwaulanga.

Akizungumzia misuli ya kampuni hiyo kiuchumi alisema Kampuni ya KingJada Hotels and Apartiment ina uwekezaji mkubwa katika nchi mbalimbali duniani na ujio wake katika jengo la Morocco Square utatoa fursa ya ajira na huduma za kihoteli.

Mradi wa Morocco Square una majengo manne ikiwemo hoteli, jengo la ofisi na jengo la nyumba kwa ajili ya makazi na maeneo ya biashara; kwenye jengo la ofisi kutakuwepo ofisi za Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambalo ni kichocheo kikubwa cha uwekezaji na ukuzaji wa mitaji kwa ajili ya maendeleo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya