Tuesday, December 24, 2024
spot_img

PRINCE HARRY KUTIKISA UFALME WA UINGEREZA

LONDON, UINGEREZA

FAMILIA ya kifalme ya Uingereza inakabiliwa na mtikisiko mkubwa baada ya mwana mfalme, Prince Harry kuandika kitabu chenye mlolongo wa malalamiko, majuto, madai na shutuma zikiwemo za matumizi ya dawa za kulevya na watoto wa Mfalme Charles kumkataa mama yao wa kambo, Camilla Parker Bowles.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya nchini Uingereza vilivyobeba dondoo za kitabu hicho na kuzua mijadala mikali wiki iliyopita, Prince Harry ameorodhesha msusuru wa madai na shutuma za kushagaza katika kitabu chake hicho kinachoitwa Spare, kilichochapishwa nchini Hispania.

Kitabu cha Spare kinatarajiwa kuanza kusambazwa Januari 10, mwaka huu lakini kimevuja kwa baadhi ya vyombo vya habari vya Uingereza kabla ya kuanza kusambazwa.

Prince Harry anakaririwa akieleza katika kitabu chake hicho kuwa yeye na kaka yake, Prince William walimsihi baba yao, Mfalme Charles asioane na Camilla, ambaye sasa ni Malkia wa Consort kwa sababu walihofia anaweza kuwa mama mbaya kwao.

Gazeti la The Sun linalochapishwa nchini Uingereza, ambalo ni moja ya vyombo vya habari vilivyoripoti dondoo za kitabu hicho, limekinukuu kuwa Prince Harry na kaka yake Prince William walifanya mikutano kadhaa ya kumjadili Camilla kabla hajajiunga rasmi kwenye familia yao ya kifalme.

Prince William na Prince Harry

Pia Prince Harry anakaririwa kuandika kwenye kitabu chake kuhusu hudhuni aliyokumbana nayo baada ya kutokea kwa kifo cha mama yake, Princess Diana na kwamba alilazimika kutafuta msaada kutoka kwa mwanamke anayemtaja kuwa, alidai kuwa ana nguvu.

Princess Diana aliuawa katika ajali ya gari iliyotokea jijini Paris nchini Ufaransa mwaka 1997 wakati Prince Harry akiwa na umri wa miaka 12.

Dondoo nyingine iliyoripotiwa kwenye katika kitabu hicho inahusu ugomvi baina ya Prince Harry na kaka yake Prince William uliotokea kwenye jumba la kifahari jijini London.

Prince Harry anakaririwa kuandika kuwa chanzo cha ugomvi huo ni maoni aliyoyatoa Prince William kuhusu mke wake, Meghan Markle kuwa ni mgumu na mkali hivyo kuibuka ubishani uliosababisha Prince William kumkwida, akakata mkufu wake wa shingoni kisha akamwangusha chini

“Aliweka glasi yake ya maji chini akaniita jina jingine kisha akaja kwangu akanikwida shingoni, akakata mkufu wangu na kuniangusha chini. Niliangikia kwenye bakuli la chakula cha mbwa ambalo lilipasuka vipande vipande mgongoni kwangu. Nililala hapo nilipoangukia kwa muda nikiwa nimepigwa na butwaa, niliposimama nilimwambia atoke nje,” anakaririwa kuandika Prince Harry.

Aidha, katika kitabu chake hicho Prince Harry anakaririwa kuandika kuwa alipata kutumia dawa za kulevya aina Cocaine alipokuwa na umri wa miaka 17 na pia alipata kutumia bangi.

Prince Harry akiwa jeshini nchini Afghanistan

“Haikuwa ya kufurahisha sana na haikunifanya nijisikie mwenye furaha kama ilivyookena kwa watu wengine lakini ilinifanya nijisikie tofauti na hilo ndilo lilikuwa lengo langu.

“Nilikuwa mvulana wa umri wa miaka 17 ambaye nilikuwa tayari kujaribu kitu chochote;” anakaririwa Harry na dondoo nyingine inazungumzia jinsi alivyopata kuvuta bangi bafuni wakati akiwa mwanafunzi katika Chuo cha Eton bila maofisa wa polisi waliokuwa walinzi wake kujua.  

Kitabu cha Spare kinazungumzia pia mauaji ya wapiganaji 25 wa kikundi cha Taliban ambapo Prince Harry anaeleza kuwa alikuwa rubani wa Helikopta ya kivita nchini Afganistan kati ya mwama 2012 hadi 2013 na alishiriki oparesheni sita za kijeshi zilizohusisha vifo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya