Tuesday, December 24, 2024
spot_img

KAMATI ZA BUNGE KUANZA KUKUTANA JANUARI 16

RIPOTA PANORAMA

KAMATI za Kudumu za Bunge zinatarajiwa kuanza kufanya vikao vyake Januari 16 hadi 29 jijini Dodoma, ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuanza kwa mkutano wa kumi wa Bunge unaoratajiwa kuanza Januari 31, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 5, mwaka huu na Kitengo cha Mawasilianio na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge, kamati mbili za kudumu za Bunge zitakutana mapema zaidi ya ratiba iliyopangwa ya kuanza kukutana kwa kamati nyingine.

Taarifa hiyo inazitaja kamati hizo za kudumu za Bunge kuwa ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.

Inazitaja shughuli zilizopagwa kufanywa na kamati wakati wa vikao hivyo kuwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa za mwaka za shughuli za kamati zilizowasilishwa bungeni Februari, 2022 na kupokea na kujadili taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za umma nchini ili kufuatilia utekelezaji wa sera na mipango ya sekta zinazohusika.

Shughuli nyingine ni kuchambua taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu kaguzi maalumu na kaguzi za ufanisi zitakazofanywa na kamati mbili za kudumu za Bunge zinazohusika kusimamia matumizi ya fedha za umma.

Katika vikao hivyo, kamati husika zitapokea na kuchambua taarifa ya uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini iwapo uwekezaji huo una ufanisi na umezingatia taratibu, sheria na miongozo mujarabu ya biashara na shughuli nyingine ni kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye wizara na taasisi mbalimbali kuhusu ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa vyanzo vya mapato na utekelezaji wa bajeti.

Taarifa inaeleza zaidi kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge Sheria Ndogo itachambua sheria ndogo zilizowasilishwa wakati wa mkutano wa tisa wa Bunge na pia kamati itapokea na kuchambua taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sheria ndogo zilizowasilishwa  katika mkutano wa tano, wa sita na wa saba wa Bunge.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya