RIPOTA PANORAMA
JESHI la Ulinzi (JWTZ) limeandaa semina itakayoshirikisha Umoja wa Mataifa (UN) na wafanyabiasha wa Tanzania inayotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Taarifa fupi kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa semina hiyo itafanyika kwa muda wa siku mbili.
Luteni Kanali Ilonda ameeleza kuwa semina hiyo itafanyikia kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichopo Knduchi jijini Dar es Salaam na itafunguliwa Januari 9, 2023 na kufungwa Januari 10, 2023 majira ya saa 7.30 mchana.