Monday, December 23, 2024
spot_img

PELE KUZIKWA JUMANNE NYUMBANI KWAKE SANTOS

MASHIRIKA YA HABARI

MWILI wa mcheza soka wa karne na mfalme wa kabumbu duniani, Edson Arantes do Nascemento – Pele unatarajiwa kuzikwa kaburini siku ya Jumanne, Januari 3, 2023 katika mji aliozaliwa wa Santos.

Kwa mujibu wa taarifa ya Klabu ya FC Santos ambayo Pele alitumia sehemu kubwa ya maisha yake kisoka akiitumikia, mazishi yake yatahudhuriwa na familia yake na jamaa wengine wa karibu na familia hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jeneza lenye mwili wa Pele litaondolewa kutoka hospitali alikoaga dunia iliyoko Sao Paulo siku ya Jumatatu na kusafirishwa kwenda Mji wa Santos ulio umbali wa kilometa 80.

Inaeleza zaidi kuwa baada ya jeneza lenye mwili wa Pele kufikishwa Santos, litawekwa kwenye uwanja wa klabu hiyo ambapo waombolezaji watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kabla ya kuzikwa kaburini siku ya Jumanne.

Leo ikiwa ni siku ya tatu baada ya Pele kuaga dunia, salamu za rambirambi zimeendelea kumiminika kutoka kwa wanasiasa, wanamichezo, wanamuziki na watu wengine mashuhuri duniani.

Salamu hizo zimekuwa zikimtaja Pele kuwa nyota ya mchezo wa kabumbu duniani iliyoziamika na katika Jiji la Rio de Janeiro picha zake zimetanda kila mahali kama ishara ya kuombeleza kifo chake.

Pele

Mchazaji nyota wa kabumbu wa Brazil wa sasa, Neymar Junior ameeleza kuwa Pele aliubadili mchezo wa soka kuwa sanaa huku kiungo mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe akisema kuwa urithi ulioachwa na Pele kwenye mchezo wa kabumbu kamwe hautasahaulika.

Cristiano Ronaldo wa Ureno yeye amemwelezea Pele kuwa alikuwa mfano wa kuigwa kwa mamilioni ya watu duniani na Nahodha wa Timu ya Argentina, Lionel Messi ambaye hivi karibuni aliiongoza timu yake kushinda kombe la dunia huko Qatar amemuomboleza Pele kwa maneno mafupi kuwa; ‘apumzike kwa amani.’

Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino yeye amemuombeleza Pele kwa kueleza kuwa rekodi yake haiwezi kuelezwa kwa ufupi kwa kutumia maneno huku Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA), Aleksander Ceferin akisema umahiri wa Pele uwanjani haukuwa na kipimo na aliendelea kuwa mtu maarufu sana hata baada ya kustaafu kusaka kabumbu.

Pele alifariki dunia Alhamis wiki hii akiwa na umri wa miaka 82 akishikiria rekodi ya mchezaji pekee wa soka kuwahi kutwaa makombe matatu ya dunia akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil mwaka 1958, 1962 na 1970.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya