Tuesday, December 24, 2024
spot_img

MKEYENGE WA TASAC AWA ‘BUBU’

RIPOTA PANORAMA

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdul Mkeyenge ameamua ‘kuwa bubu’ kuzikalia kimya tuhuma za kutumia ‘njia za panya’ kuipatia Kampuni ya Mas Holding and Container Depot Limited, leseni ya kufanya biashara ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha kontena.

Ikiwa ni takriban mwezi mmoja sasa tangu alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo ikiwa nia pamoja na kufikishwa maswali yanayoombewa majibu na ufafanuzi kwa msaidizi wake, Josephine Bujimu anayehusika na utoaji taarifa; na huku kukiibuka madai mapya yanayomuhusisha moja kwa moja Mkeyenge na skandali hiyo, Mkeyenge hapokei simu wala kujibu ujumbe wa maandishi unaotumiwa kwenye simu yake kiganjani.

TASAC na Mkeyenge wanahusishwa na skandali ya kutoa leseni ya biashara ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha kontena kwa Kampuni ya Mas Holding and Container Depot Limited huku ikiwa haina vifaa vya kupokea na kupakia kontena na aidha;

Wanahusishwa na utoaji leseni hiyo bila kufanya ukaguzi kwenye eneo ambalo Kampuni ya Mas Holding and Container Depot Limited iliomba kufanyia biashara; aneo ambalo kuna biashara nyingine ya uhifadhi wa kontena tupu za wenye meli.

Kwa mujibu wa sheria, TASAC ni mdhibiti wa masuala yahusuyo shughuli na biashara za usafirishaji baharini na moja ya majukumu yake ni kukagua eneo na vifaa vya biashara linaloombewa leseni kabla ya kutoa leseni.

Pia kuhakikisha eneo husika na wahusika wana vigezo vilivyowekwa na kuhakikisha muombaji anavyo vifaa kama vile vya kupokea na kupakia kontena kabla ya kutoa leseni. Taratibu zote hizo zinadaiwa kukiukwa na Mkeyenge na TASAC.

Inadaiwa, kabla ya kutolewa kwa leseni hiyo, Mkeyenge alifikiwa kwanza kwa mazungumzo binafsi na waombaji hao ambao mbali na skandali hii, pia wanaandamwa na skandali ya kupoka mali za Serikali kwenye Kampuni ya Mwananchi Engineering and Contracting Company Limited (MECCO) na kuzitumia kuchukulia mkopo mkubwa Benki ambao hadi sasa wameshindwa kuulipa.   

Taarifa za ndani kuhusu skandali hii zinadai kuwa TASAC huku ikijua kuwa mwombaji leseni, Kampuni ya Mas Holding and Container Depot Limited hana vifaa vya kupokea na kupakia kontena ambavyo ni kigezo cha kumuwezesha kupewa leseni aliyoomba; baada ya kuketi kwa mazungumzo na Mkeyenge leseni ya biashara ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha kontena ilitolewa kwa mwombaji huyo.

Inadaiwa zaidi kuwa leseni hiyo ilitolewa bila kufanya ukaguzi kwenye eneo ambalo Kampuni ya Mas Holding and Container Depot Limited iliomba kufanyia biashara; madai ambayo Mkeyenge na wasaidizi wake wameshindwa kuyatolea kauli kwa takriban mwezi mzima sasa.

Novemba 28, 2022 Tanzania PANORAMA Blog ilifika TASAC, ofisini kwa Mkeyenge ikiwa imefumbata maswali mawili mkono kuhusu ukiukwaji huo wa uratatibu wa utoaji leseni uliofanywa na ofisi yake kwa ajili ya kumuuliza naye ayajibu na kukutana na Katibu Muhtasi wake ambaye alieleza kuwa bosi wake hayupo lakini mwenye dhamana ya kujibu maswali ya waandishi wa habari kwa niaba ya bosi huyo ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Habari na Mawasiliano, Josephine Bujimu.

Bujimu alizungumza na Tanzania PANORAMA Blog na kuomba atumiwe maswali yanayoombewa majibu na ufafanuzi kwenye simu yake ya kiganjani ili atakapomaliza kikao ayajibu na Tanzania PANORAMA Blog ilimtumia maswali Bujimu kama alivyoomba na yeye;

Novemba 29, 2022 mapema saa 1.26 asubuhi, aliandika kukiri kuyapokea, “Nimepokea. Asante sana …. Good morning.” Baada ya kutuma ujumbe huo hakupatikana tena licha ya kukumbushwa mara kadhaa kujibu, lakini kila simu yake ilipoita, haikupokelewa.

Novemba 30, 2022 Tanzania PANORAMA Blog iliendelea kumtafuta Bujimu bila mafanikio kwani licha ya simu yake kuita lakini haikupokelewa na Disemba Mosi, 2022 alipopigiwa kwa namba nyingine ya mtandao wa tigo alipokea kwa bashasha lakini baada ya kuelezwa kuwa anazungumza na Tanzania PANORAMA Blog, alipunguza sauti na kuwa ya chini sana kisha akasema yupo kwenye kikao hawezi kuongea lakini majibu yapo tayari hivyo baada tu ya kikao atayatuma.

Bujimu hakutuma majibu kama alivyoahidi na tangu siku hiyo hakupokea tena simu ya Tanzania PANORAMA Blog wala kujibu ujumbe alioandikiwa.

Baada ya kutafutwa kwa muda mrefu, Disemba 10, 2022 Bujimu alipatikana na kudai kuwa bado hajapata majibu ya maswali aliyoulizwa na kuahidi kuwa yatakuwa tayari Disemba 12 na alipotafutwa siku hiyo alisema hawezi kuahidi kuyatoa kwa sababu yupo kwenye kikao JNICC.

Alipotafutwa jana alisema apewe muda mfupi awasiliane na wakubwa ili atoa majibu lakini hakurejea kutekeleza ahadi yake hiyo.

Kwa upande wake Mkeyenge, licha ya kuelezwa na baadhi ya watu walio karibu na ofisi yake kuwa yupo ofisini lakini hataki kuonana na waandishi wa habari kuzinguzia skandali hiyo, kila anapotafutwa simu yake inaita bila kupokelewa na akitumiwa ujumbe kwenye simu yake ya kiganjani anausoma lakini hajibu chochote.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya