Tuesday, December 24, 2024
spot_img

CHINA, TANZANIA ZASAINI HATI 15

RIPOTA WA RAIS

Rais Samia Suluhu Hassan jana alishuhudia utiaji saini wa mikataba na hati za makubaliano ya kimkakati 15 iliyolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji wa baina ya Tanzania na China.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus tukio hilo lilishuhudiwa pia na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping.

Taarifa ilieleza kuwa miongoni mwa mikataba hiyo inalenga kuipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Sh bilioni 31.4 inayodaiwa na China.

Ilieleza zaidi kuwa miongoni mwa mikataba na makubaliano yaliotiwa saini ni kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China.

Mkataba mwingine unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu baina ya Tanzania na China.

Aidha, yalisainiwa makubaliano kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa mabondo ya samaki pamoja na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China.

Taarifa ilieleza kuwa China imetoa mkopo kwa Tanzania wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, Terminal II.

China inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania na hadi kufikia Oktoba 2022, jumla ya miradi 1,098 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 9.6 ilisajiliwa katika kituo cha uwekezaji cha TIC.

Miradi hiyo imezalisha ajira 131,718 katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano, madini na uvuvi.Rais Samia yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali kwa mwaliko wa Rais Jinping na ameishakutana na Waziri Mkuu wa China na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Rais Samia yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali kwa mwaliko wa Rais Jinping na ameishakutana na Waziri Mkuu wa China na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya