Monday, December 23, 2024
spot_img

MASHINE 300 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA ZATEKETEZWA

RIPOTA PANORAMA

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini (GBT) imeendesha msako na kukamata mashine za michezo ya kubahatisha 300 ambazo zilikuwa zinatumika kuikosesha serikali kiasi cha Sh milioni 400 kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa mashine hizo katika dampo la taka za kielektroniki lililopo Kisarawe, mkoani Pwani hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa GBT, James Mbalwe amesema kuwa mashine hizo zimepatikana baada ya kuendesha opereshini maalum katika mikoa saba.

Amesema baada ya kufanya msako huo katika mikoa ya Lindi, Pwani, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro Manyara na Songwe, mashine hizo zilizokuwa na thamani ya Sh milioni 300 zilikamatwa ambapo sheria zinaelekeza kwua zinatakiwa ziteketezwe.

Akieleza sababu za kukamatwa kwa mashine hizo, Mbalwe ambaye alikuwa ameambatana na maofisa ukaguzi wa Bodi hiyo amebainisha kuwa mashine hizo zilikamatwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanya biashara bila leseni, kuingizwa nchini kinyemela, kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa pamoja na kukwepa kodi.

“Kwa ujumla mashine hizi zinapoteza jumla ya Sh milioni 33 kwa mwezi sawa na takribani Sh milioni 400 kwa mwaka.

“Pamoja na kukwepa kodi na tozo mbalimbali, waendeshaji haramu pia wamekuwa wakiwaruhusu Watoto wadogo kushiriki kinyume na Sheria,” Mkurugenzi huyo ameeleza.

Hata hivyo, jumla ya watu wanane wamekamatwa katika opereshini hiyo iliyotetekelezwa katika miezi ya Julai na Agosti, mwaka huu na tayari wameshafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ameongeza kuwa bodi hiyo imekuwa ikiendesha operesheni maalum mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha kuwa michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kuleta tija katika maendeleo ya taifa na kuepusha jamii na athari hasi.

Hata hivyo, ameishukuru Mamlaka ya Mapato (TRA) na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Bodi hiyo kutika zoezi hilo huku akiwataka viongozi wa maeneo mbalimbali kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa mchezo huo unakuwa tija kwa taifa.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya