Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchini (LATRA), imeendelea kusisitiza kuwa inazidi kujikita katika kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza mamlaka hiyo, kwakuwa kwa kufanya hivyo wanaamini watachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani na madhara yake nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Habib Suluo, hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mabalozi na Kongamano la Usalama Barabarani 2022