Monday, December 23, 2024
spot_img

DENDEGO: CHANGAMKIENI FURSA ZA UTALII

RIPOTA PANORAMA

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amewataka wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za utalii kufuatia Kongamano la Kimataifa la Utalii litakalofanyika katika viwanja vya Kihesa Kilolo.

Kongamano hilo litakaloanza Novemba 9-13 limelenga kufungua milango ya utalii Kusini mwa Tanzania na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika mikoa 10.

Mikoa inayoshiriki kongamano hilo ni Iringa, Mbeya, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Njombe, Songwe na Morogoro.
Akizungumza na wanahabari mkoani Iringa, Dendego amesema hiyo ni nafasi adhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Iringa kuchangamkia fursa za kiutalii.

Amesema wananchi wanaweza kutumia kongamano hilo kuuza bidhaa zao mbalimbali ikiwemo vyakula.

“Hili ni kongamano lenye hadhi ya Kimataifa kwa hiyo Changamkieni huu fursa,uwe mfanyabiashara mdogo au mkubwa nafasi ipo,” amesema Dendego.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makumbusho ya Mkoa wa Iringa, Jimson Sanga amesema kongamano hilo litasaidia kukuza sekta ya utalii kwenye mikoa hiyo.

Amesema pia litaongeza ari ya wageni kutembelea vivutio vya kitalii vinavyo patikana katika mikoa hiyo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya