MOGADISHU, SOMALIA
MJI mkuu wa Somalia Mogadishu umekumbwa na milipuko miwili mchana huu.
Moshi mweupe unaweza kuonekana ukifuka karibu na ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.
Moja ya milipuko hiyo inaripotiwa kukumba afisi za Wizara ya Elimu.
Hata hivyo hadi kufikia sasa, hakuna taarifa zozote zilizotolewa zinazoangazia idadi ya watu waliojeruhiwa.
Na pia, hakuna aliyedai kuhusika na milipuko hiyo.