Monday, December 23, 2024
spot_img

ENDELEENI KUFICHUA UKATILI KWA WATOTO

RIPOTA PANORAMA

WAKATI taasisi ya Save the Children, ikizindua dawati la ulinzi wa mtoto Shule ya Msingi Levolosi jijini Arusha na mabaraza ya watoto kwa lengo kupata taarifa za ukatili wanazofanyiwa watoto, vyombo vya habari vimeaswa kuendelea kufichua maovu wanayofanyiwa watoto, ili kuisaidia serikali kukomesha matukio hayo.

Akizungumza na watoto jana jijini Arusha, Mratibu wa Jinsia kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Linus Kahendaguza,​ alisema endapo vyombo vya habari vikiendelea kuandika na kuibua aina za ukatili wanaofanyiwa watoto na wanawake maeneo mbalimbali, itakuwa rahisi wahusika kuchukuliwa hatua.

Amesema serikali itaendelea kuzindua madawati hayo shuleni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwemo taasisi zisizo za kiserikali, ili kudhibiti ukatili wanaofanyiwa watoto nyumbani na shuleni.

“Vitendo vya ukatili vinavyotolewa taarifa ni asilimia 12​ pekee, hivyo wanahabari wana wajibu wa kuendelea kuandika na kuibua changamoto zinazowakabili wanawake na watoto pamoja na makundi maalum, ili kutokomeza madhila wanayofanyiwa,” amesema.

Kwa upande wake Wilbert Muchunguzi, ambaye ni mtaalam wa haki za watoto kutoka shirika la Save the Children, amesema shirika hilo litaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa watoto, ili wajue haki zao na wapi pa kuzipata, ili kudhibiti ukatili hasa shuleni, nyumbani, ikiwemo kupinga unyanyasaji wa kimwili.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya