Tuesday, December 24, 2024
spot_img

WAZIRI MKUU ZIARANI KOREA KUSINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na viongozi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla hajaondoka  kwenda Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi.  Kulia ni Mkewe, Mary Majaliwa, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James na wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk. (Picha  kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu)

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo kwenda Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha Ofisi ya Waziri Mkuu, akiwa Korea Kusini atakutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Han Duck-soo. Pia anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda na vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.

Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha uhusiano na Korea Kusini ambao umedumu kwa miaka 30 na pia kukuza uhusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, uhusiano wa anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya