Wednesday, December 25, 2024
spot_img

‘WANASIASA MWACHENI AKWILINA APUMZIKE KWA AMANI’

RIPOTA PANORAMA

WANASIASA wameonywa kuutumia kisiasa msiba wa mwanafunzi Akwilina Akwilini na badala yake wametakiwa kumuacha apumzike kwa amani.

Akwilina aliuawa mwezi uliopita baada ya kupigwa risasi wakati polisi wakitawanya maandamano ya wanachama na mashabiki wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Mbali na wanasiasa, wengine walioonywa kuacha kuutumia msiba huo kwa malengo yao ni makundi ya wanaharakati yanayotumia mwamvuli wa wanasiasa.

Onyo hili limetolewa jana na Mwenyekiti Jumuiya ya Taasisi za Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), George Mnali katika mkutano wa kamati tendaji ya umoja huo. Kamati hiyo iliketi jana kujadili changamoto zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu.

Mnali alisema TAHLISO inaelekeza lawama kwa makundi matatu kwa tukio hilo aliyoyataja kuwa ni wanasiasa, wananchi na waliozuia maandamano hayo ambayo yaligharimu uhai wa Akwilina.

Alisema wanasiasa wanapaswa kuchunga kauli zao, waangalie wanazungumza nini na wapi kwa sababu Taifa linataka amani.

Mnali alisema onyo hilo halilenga kundi lolote la wanasiasa bali linawahusu wote na kwamba waliozuia maandamano na kuibua ghasia walipaswa kuwa makini kwa sababu katika maandamano yale kilichotakiwa ni kuzuia tu.

“TAHLISO ndio chombo kikuu cha kuwasemea wanafunzi wote nchi nzima, hakuna mwingine. Tambua kuna kifo cha mwanafunzi mwenzetu Akwilina aliyekuwa anasoma Chuo cha Usafirishaji lakini kuna vikundi vimejitokeza kutoa matamko mbalimbali.

“Vikundi vingine vimeenda mbali zaidi kwa kuwataka baadhi ya watendaji kujiuzulu wakati uchunguzi bado unaendelea na matokeo
hayajatoka, inaashiria vinatumika kisiasa,” alisema Mnali

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya