Saturday, May 31, 2025
spot_img

WACHONGA VINYAGO KUPEWA ENEO UWANJA WA MKAPA

RIPOTA PANORAMA

SERIKALI itawapatia eneo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, wasanii wa sanaa za uchongaji vinyago, uchoraji na sanaa nyingine za ubunifu ili wapate nafasi kubwa ya kuonyesha kazi zinazoakisi utamaduni wa Mtanzania.

Hayo yameelezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas katika mkutano wake na wadau wa sanaa za ufundi jijini Dar es Salaam.

Dk. Abbas alisema kupatikana kwa eneo hilo kutatoa nafasi kwa wasanii kuuza kazi zao kwa wingi kwa watanzania na raia wa kigeni kila kunapotea michezo inayozishirikisha timu za mpira wa miguu za ndani na nje.

Alisema Serikali pia itasimamia kivitendo hoja ya wasanii hao ya kutaka watanzania wengi watumie kwa wingi sanaa za uchongaji, uchoraji na nyinginezo za wasanii wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, Dk. Abbas alitembelea kituo cha ubinifu sanaa za muziki, Tanzania House of Talents (THT) ambako alisema Serikali haitakiacha kamwe bali itashiriki kwa karibu kuhakikisha malengo ya kuanzishwa kwake yanaendelezwa.

Akizungumza na wasanii wa THT katika kituo hicho kilichoasisiwa na marehemu Ruge Mutahaba alisema wizara yake itakiunganisha kituo hicho na Chuo cha Sanaa na Utamaduni, Bagamoyo.

0711 46 49 84

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya