Saturday, May 31, 2025
spot_img

TANZANIA INA WATU THABITI AFRIKA – DK. ABBAS

RIPOTA PANORAMA – 0711 46 49 84

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas emesema watanzania ni watu thabiti na wenye historia ya kutukuka katika mapambano ya ukombozi wa Bara la Afrika.
Dk. Abbas ameyasema hayo jana alipotembelea makao makuu ya Ofisi za Ukombozi wa Bara la Afrika kujionea changamoto zinazoukabili.

Akizungumza katika ofisi hizo, alisema Tanzania ni nchi yenye watu wenye historia thabiti barani Afrika kutokana na kushiriki kikamilifu kuzikomboa nchi nyingi barani humo.

“Tanzania si tu imetoa mchango mkubwa katika historia ya ukombozi wa Afrika bali imegharamika mno kuanzia watu wetu, fedha zetu na hata kuiweka nchi yetu katika hatari ya kushambuliwa.

“Viongozi wetu walifanya uthubutu mkubwa na sisi leo sio watu poa, tuko imara kuilinda nchi yetu na sisi tuliopewa dhamana ya mradi huu lazima tutimize wajibu wetu ili kuitunza historia hii na kuwajengea vijana wa sasa uzalendo na utamaduni wa kuwa watu wa kuthubutu kwa ajili ya nchi yao na Afrika,” alisema Dk. Abbas.

Alisema kutokana na umuhumu wa ofisi hizo ambazo Umoja wa Afrika (AU) uliamua makao makuu yake yawe Dar es Salaam na Serikali imeuweka chini ya usimamizi wa Idara ya Utamaduni katika Wizara ya Habari sasa unahamishwa kutoka Idara ya Utamaduni na kuwa moja kwa moja chini ya ofisi yake.

“Tunataka kwenda kasi na kwa viwango, wazee wetu walithubutu kufanya mambo makubwa kutufikisha hapa tulipo sasa naona mnafanya kazi kubwa lakini mradi huu bado una changamoto nyingi ambazo Idara ya Utamaduni pekee haiwezi kuzipeleka kwa kasi, watabaki washauri wa kitaalamu tu kwangu na kwa mradi huu, lakini kuanzia leo 7, Disemba, 2020 mratibu wa mradi huu atawajibika na kuripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,” aliagiza Dk. Abbas

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya