RIPOTA PANORAMA – 0711 46 49 84
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anaweza kufungwa gerezani kifungo cha mpaka miaka miwili iwapo Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga ataondoa huruma yake dhidi ya tuhuma za kutenda kosa alilolifanya yeye na wenzake la kudharua kwa makusudi nembo ya Taifa.
Hilo limebainika katika uchunguzi wa Tanzania PANORAMA Blog kuhusu makosa yanayoangukia kwenye kifungu namba saba cha sheria ya Nembo ya Taifa ambayo Mbowe na wenzake waliyafanya wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Chadema wa kumchagua mgombea urais na makamu wake Mwaka 2020, katika ukumbi wa Mlimani City siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni zilizodumu kwa siku 60.
Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa katika mkutano huo uliohudhuliwa pia na Tundu Lissu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, Lazaro Nyalandu ambaye ni waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbowe ambaye alikuwa Mbunge katika Bunge la 11 waliimba wimbo wa Taifa huku yeye na wenzake hao wakiongezea maneno ambayo hayapo kisheria kwenye wimbo wa Taifa.
Kwa mujibu wa sheria, kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria namba saba kwa kuufanyia dhihaka wimbo wa Taifa na wahusika wanaweza kushtakiwa mahakamani.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga, mapema wiki hii ameeleza kuwa hakuamuru kukamatwa kwa Mbowe na wenzake kwa kutanguliwa na busara ya kutoleta sintofahamu katika Taifa kipindi cha uchaguzi mkuu
Imeelezwa na baadhi ya wachambuzi wa mambo waliohojiwa na Tanzania PANORAMA Blog kuwa wakati wote wa kampeni na kipindi cha uchaguzi mkuu, maadui wa Taifa na hasa mataifa ya mabeberu walilenga kuibua hekaheka ambazo zingezaa machafuko na kuifanya nchi isitawalike, yakiwatumia wanasiasa wa ndani wanaoishi katika mataifa hayo.
Wachambuzi hao wa mambo wameeleza kushangazwa na kile walichokiita chokochoko za Mbowe kwa DPP Mganga zinazomtaka kutokuwa na huruma na wale wote waliotenda kosa la kudharau kwa makusudi nembo ya Taifa.
Mwishoni mwa mwezi uliopita baada kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi kusikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la wabunge 19 wa viti maalumu wa chama hicho, Mbowe alikaririwa kutamka maneno yenye mwelekeo wa kutaka mmoja wa wabunge hao aliyekuwa akishtakiwa kwa kosa la kudharau nembo ya Taifa arejeshwe gerezani. Mbunge huyo aliachiwa kwa mamlaka aliyonayo DPP kisheria.
Julai 4, 2020, Mbunge huyo akiwa katika Kijiji cha Puma, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida alitenda kosa la kuimba wimbo wa Taifa huku akiongeza maneno ambayo hayamo kisheria kwenye wimbo huo huku akipandisha bendera ya Chadema