Saturday, July 19, 2025
spot_img

KUFA KWA MAGAZETI YA NHL KWAIBUA UPYA MACHUNGU YA WANAOIDAI

RIPOTA PANORAMA – 0711 46 49 84

MATUMAINI ya waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd na awali kifahamika kwa jina la Habari Corporation Ltd ya kulipwa mafao yao baada ya kuondolewa kazini yamezidi kutoweka baada ya kutolewa tangazo na kusitishwa kwa uchapishaji wa magazeti yanayozalishwa na kampuni hiyo kwa sababu ya ukata.

Tangazo la kusitishwa kwa uchapishaji wa magazeti yaliyokuwa yakizalishwa na New Habari (2005) Ltd ya Mtanzania, Rai, Dimba na Bingwa lilitolewa jana katika mitandao ya kijamii ikimkariri Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky akiwatangazia wafanyakazi wanaodaiwa kuhusu kusitishwa kwa uchapishaji wa magazeti hayo.

Taarifa ya kusitishwa kwa uzalishaji wa magazeti hayo ilisomeka; “Kampuni ya New habari 2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na Dimba imetangaza kusitisha uzalishaji wa magazeti yote kutokana na mwenendo mbaya wa kibiashara.

“Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky amesema uzalishaji wa magazeti hayo utasitishwa kuanzia jumatatu ijayo.”

Muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, zaidi ya watu 150 waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni New Habari waliopunguzwa bila kulipwa mafao yao ingawa walikuwa wakikatwa kila mwezi, walianza kuelezea hisia zao huku wakieleza kuwa hatua hiyo imeibua upya machungu ya kupoteza haki zao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari, Erasto Matasia alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia suala hilo alisema yuko msibani na kwamba aliyeteuliwa na kampuni kuzungumzia usitishwaji huo na kupunguzwa wafanyakazi kwa niaba ya Hussein Bashe ni Msacky.

“Mimi sipo huko, niko msibani, nakushauri mtafute Dennis Msacky aliyeteuliwa na kampuni kulizungumzia jambo hilo kwa niaba ya Bashe,” alisema Matasia.

Jitihada za kumpata Msacky hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake ya kiganjani kuwa anaizima kila alipopigiwa na kuita.

Kampuni ya New Habari na kabla ya hapo ikifahamika kwa jina la Habari Corporation inaandamwa na madeni makubwa ya miaka mingi ya waliokuwa wafanyakazi wake ambao walikuwa wakikatwa fedha za mafao pensheni lakini zikawa hazipelekwi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Bashe, ambaye kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 LTD, amepata kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akikiri kuchota fedha za kampuni hiyo na kuzitumia katika biashara zake binafsi na kwamba alikuwa na matarajio ya kuzirejesha baada ya kupata faida.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya