RIPOTA PANORAMA
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umemtaka Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba kupima kauli zake za kuishutumu Serikali kwa sababu haziendani na umri wake.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka ndiye aliyetoa kauli hiyo jana alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC.
Katika mahojiano hayo, Shaka alisema huenda Dk. Bisimba amefurahishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka damu imwagike au yatokee mauaji kama ya Misri na Libya.
Shaka alisema anaamini Dk. Bisimba ni msomi mwenye upeo, mchambuzi hodari na mtetezi wa masuala ya kisheria hivyo hapaswi kufumbia macho kauli za Mbowe.
āMama yetu nadhani sasa ameanza kuzeeka. Amepoteza uwezo wake mkubwa wa kupambanua mambo kwa kutazama haki na usawa. Nasita kumwita mshabiki badala ya kuwa mtumishi bora wa jamii.
āTunafahamu kituo cha sheria kimekuwa kikitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kuendesha mikutano ya kiharakati, kushinikiza mapambano dhidi ya Serikali pia mara kadhaa kutaka kukivuruga chama tawala. Tumewatambua na katu hatutawaonea aibu,ā alisema Shaka.
Alimtaka Dk. Bisimba kueleza uhuru mpana wa vyombo vya habari uliopo nchini unapatikana sehemu gani katika Bara la Afrika hata atamke umepotea nchini.