RIPOTA PANORAMA
WATANZANIA 14 waliokamatwa na madawa ya kulevya katika nchi mbalimbali duniani wamenyongwa hadi kufa.
Sambamba na hao, Watanzania wengine 12 waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara hiyo wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia Blog hii kutoka Kitengo cha Dawa Kulevya Zanzibar, walionyongwa ni Juma Omar Mgeni ambaye hajatatwa makazi yake, Masumbuko Salum Hassan mkazi wa Dar es Salaam, Salum Mohammed Kitupura mkazi wa Dar es Salaam, John James Amandus mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, Bantulaki Isihaka Ally mkazi wa Tanga na Zungiza Mohamed Ally mkazi wa Dar es Salaam.
Wengine walionyongwa ni Farida Sarboko Makarani mkazi wa Zanzibar, Said Mfaume Said ambaye haijatajwa makazi yake, Mohammed Bakari Mkemi, haijatajwa makazi yake na Mariam Ramadhan Mahimbo ambaye haijatajwa ni mkazi wa wapi.
Wengine walionyongwa ni Julieth Jonathan Jaspher, haijatajwa makazi yake, Halifa Matumla Ally, haijatajwa makazi yake, Rajabu Salum Mwanyenza, haijatajwa makazi yake na Hamisi Kombo Ally.
Waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani ni Rashid Mzonge mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, Salum Jumbe Pigigi haijatajwa makazi yake, Luka Joseph Urio mkazi wa Dar es Salaam, Masome Frorian Anthony mkazi wa Dar es Salaam na Mwanjati James Simon mkazi wa Dar es Salaam.
Wengine waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani ni Mohammed Musa Mohammed mkazi wa Dar es Salaam, Yahya Ally Seif mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Chande Mohammed Chande mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam na Rashid Bakari Mzonge mkazi wa Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Orodha hiyo inawataja pia Mende Katija Mikidadi mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam, Shame Shame Udai mkazi wa Dar es Salaam, Mlenzi Mangala Hamisi mkazi wa Dar es Salaam na Ismail Mohammed Rajabu Mapusa mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam.
Waliofungwa katika magereza mbalimbali na vifungo vyao katika mabano ni Abdallah Ally Rashid Mbonde Fredue mkazi wa Dar es Salaam (15), Mzia David Michael mkazi wa Dar es Salaam (22) na Ramadhan Iddi Juma mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam (7).
Wengine ni Saleh Happy Hambona mkazi wa Dar es Salaam (18), Michael Dalasi Taraja mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam (19), Begge Hemed Ahmed mkazi wa Tanga (15) na Omalla Donald Nyowino mkazi wa Dar es Salaam (15).
Katika orodha wamo pia Adam Hariri Mohammed mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam (18), Bakari Badi Omari Mneko mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam (17), Masomi Thomas Joseph mkazi wa Dar es Salaam (17), Abdallah Iddi Ally mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam (17), Kondo Ally Mohammed (20), Mohammed Abubakar Nazzir (24) na Abdallah Anwar Abasi (24) ambao haijatajwa makazi yao.
Orodha inawataja pia Makuti Al- Jaribu Hassan mkazi wa Kilwa mkoani Lindi (25), Abdallah Iddi Athuman (24) ambaye makazi yake hayajatajwa, Mnyamani Hamad Ally mkazi wa Tanga (22), Mtalu Rajabu Ally Rajabu mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam (17) na Shughuli Kibaya Bakari mkazi wa Tanga (8).
Inawataja pia Mfaume Omar Ng’anzi Msuya mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam (21), Steven Robert Onay (9) na Omar Juma Mang’enge (8) ambao makazi yao hayajatwa, Steven Simon Kanul mkazi wa Dar es Salaam (8), Iddi Haji Fumo mkazi wa Unguja (9), Seleman Hamisi mkazi wa Unguja (8) na Athuman Hassan Nash mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam (8).
Pia Seleman Hussein Msimbe (8) ambaye makazi yake hayajatajwa, Abdallah Farid Twalib mkazi wa Dar es Salaam (17), Salim Ally Amani, makazi yake hayajatajwa (22), Calist Wilson Mosha mkazi wa Arusha (18), Saleh Abdul Omar mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam (21), Bugingo Sweetbert Rwezaura mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam (21) na Mohammed Omari Ally mkazi wa Zanzibar (19).
Orodha inawataja wengine kuwa ni Sayula Rashid Paul ambaye makazi yake hayajatajwa (16), Koshuma Geofrey Gabriel mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam (30), Salim Mrisho Hussein mkazi wa Tanga (21), Riziki Riziki Hamduni mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam (19), Bashir Rajabu Kafune mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam (19), Kharim Mohammed Omar mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam (19), Abubakar Abdul Ligalwike mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam (8) na Pendo Ernest Kessy mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam (9).
Watanzania waliokamatwa sehemu mbalimbali duniani wakiwa na dawa za kulevya wanaosubiri kuhukumiwa ambao majina yao yako kwenye kitengo cha dawa za kulevya Zanzibar, lakini haijatajwa sehemu wanazoishi ni Sephu Abdulrahman, Alfredy Thomas Singini, Lawrence Mbogoni Oni, Mohammed Ibrahimu Kilima, Wilfred Casmir Mushi na Shakira Ahmed Mumba.
Wengine ni Jackline Benedict, Rajabu Rashidi Mshare, John Peter Martin, Abdallah Mwalimu Mbaruk, Rashid Mzee Mrisho, Juma Ismail Nayopa, Tsakiris Costa Achelis, Faith Michael Kabambe.