Thursday, May 15, 2025
spot_img

Filamu tatu za Tanzania zachomoza kimataifa

Filamu tatu za Tanzania zimepata nafasi kuoneshwa kwenye mtandao wa kimataifa wa kuonyesha filamu wa Netflix.

Hayo yamesemwa na Meneja Mipango na Masoko kutoka Bodi ya Filamu, Goodluck Chuwa, wakati wa ukusanyaji kazi za wasanii wa filamu kwa ajili ya kushiriki kwenye tuzo za filamu Tanzania mwaka 2022.

Amesema kuwa filamu hizo ni Binti, Bahasha pamoja na Nyara, ambazo zimeweza kufanya vizuri kimataifa kutokana na kutengenezwa kwa viwango vyenye ubora.

“Filamu hizo ni sehemu ya kielelezo kwamba sasa soko la filamu zetu limekua na wasanii wetu kutoa kazi ambazo zina ubora mkubwa hadi kushindanishwa kimataifa,”amesema Chuwa.

Naye Ofisa Utamaduni Mkoa wa Tanga, Emmanuel Makene amewataka wasanii wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye tuzo hizo.

Jumla ya vipengele 31 vinashindaniwa katika tuzo hizo, huku mwisho wa kuwasilisha kazi za wasanii ikiwa ni Oktoba 30 mwaka huu.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya