Tuesday, December 24, 2024
spot_img

BENZEMA: sioni sehemu sahihi ya kustaafia zaidi ya Real Madrid

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Uhispania, Karim Benzema, amesema anatarajia kustaafu soka akiwa na miamba hao wa soka barani Ulaya, kwa kile alichosema kuwa haoni sehemu nyingine sahihi ya kwenda nje ya miamba hao.

Benzema, ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliokuwa wakifanya mahojiano naye muda mfupi baada ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, katika tuzo za mwaka huu.

Tuzo hiyo imefuatia mshambuliaji huyo kuwa na moja ya misimu bora kabisa katika maisha yake ya soka, ambapo msimu uliopita aliiwezesha Madrid kutwaa ubingwa wa Ulaya na ule wa Hispania, kutokana na mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya miamba hao.

Amesema kwamba, anajua kuna vilabu vingi ambavyo vingetamani akachezee, lakini anaamini kuwa Madrid ndio sehemu sahihi kwake kumalizia soka lake.Benzema mwenye miaka 34 hivi sasa, alisajiliwa na Madrid mwaka 2009, wakati huo akitajwa kuwa mmoja wa washambuliaji makinda waliotarajiwa kuonyesha maajabu baadae.

Hata hivyo, kwa miaka yote hiyo, ni kama alikuwa akifunikwa na kivuli cha Cristiano Ronaldo, ambaye alikuwa mfalme wakati akiwa Madrid, lakini toka mreno huyo aondoke katika ardhi ya Hispania, Benzema ameibuka kuwa mchezaji muhimu na nguzo kuu ya Real Madrid, huku akionyesha ubora wa hali ya juu katika kila mechi anayocheza.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya