Tuesday, December 24, 2024
spot_img

WAZIRI MKUU AUNGANA NA MAMIA KUMUAGA MREMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Marehemu Augustino Mrema, leo.


RIPOTA WA WAZIRI MKUU 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kumkumbuka Marehemu Augustino Lyatonga Mrema kutokana na mchango wake mkubwa wa kuendeleza mahusiano na vyama vya siasa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na mamia ya waombolezaji kwenye ibada ya kumuaga marehemu Mrema katika Parokia ya Mtakatifu Augustino Kilimahewa, Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Mrema atakumbukwa kama kiongozi mkuu wa Chama cha TLP kwa muda mrefu sana. Na akiwa katika siasa, aliisaidia Serikali kupata mwelekeo mzuri wa vyama vya siasa,” amesema Waziri Mkuu.

Amesema salamu za Rais Samia Suluhu Hassan, ziliwasilishwa asubuhi na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.

“Sisi tuliopo hapa tuna mambo mawili makubwa ya kufanya ili kumuenzi ndugu yetu Mrema. Moja ni kuenzi yale yote aliyofanya kwa upande wa Serikali na upande wa siasa lakini pili, tuendelee kumuombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuilaza roho yake mahali pema peponi,” amesema.

Kuhusu mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi huko Kiraracha, Moshi, Waziri Mkuu amesema Serikali itawakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.

Akizungumza na niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo, DCP Anthony Luta alisema Jeshi la Polisi litaendelea kumkumbuka Mrema kwa mambo kadhaa ikiwemo hatua yake ya kuanzisha jeshi la ulinzi wa sungusungu, ujenzi wa vituo vidogo vya polisi na utetezi wa haki za wanawake ambapo kwa sasa wameanzisha madawati ya jinsia kwenye vituo vya polisi.

Naye Paroko wa kanisa hilo, Padre Peter Assenga alisema Mrema alikuwa akijitolea kwa mambo mengi parokiani hapo na ataendelea kukumbukwa sana.

Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu alisema umati mkubwa uliokuwepo kanisani hapo ni ishara tosha ya jinsi Mrema alivyoishi vizuri na watu wakiwemo viongozi wa Serikali na vyama vya siasa.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu mmoja na mapadre sita. Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Hamad Rashid, Prof. Ibrahim Lipumba, John Cheyo, Steven Wassira, James Mbatia, Joseph Selasini na Mchungaji Dk. Eliona Kimaro.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA TANZANIA LABOUR PART (TLP) MAREHEMU AUGUSTINO MREMA. MWILI WA MAREHEMU MREMA AMEAGWA LEO KATIKA KANISA LA MTAKATIFU AUGUSTINO, LILILOPO SALASALA, DAR ES SALAAM NA UNATARAJIWA KUZIKWA KESHO HUKO KIRARACHA MKOANI KILIMANJARO. 


 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya