MKUU wa Wilaya ya Ikungi (DC), mkoani Singida, Jerry Murro leo amehitimisha utoaji elimu ya sensa ya watu na makazi katika Kata ya Siuya kwa kuwaomba wananchi kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa ya watu na makazi watakapofika katika makazi yao.
Murro amewaambia wananchi wa Kata ya Siuya kuwa Serikali imeamua kuwafikia kuwapa elimu ya sensa ikitambua thamani ya kila mwananchi kushiriki sensa ya watu na makazi bila kujali itikadi za kisiasa, dini wala kabila.