Tuesday, December 24, 2024
spot_img

ACT WAZALENDO YAITAKA SERIKALI KUSITISHA TOZO ZA HUDUMA ZA KIBENKI

Naibu wa Sekta ya Fedha na Uchumi wa Chama cha ACT Wazalendo, juma Kombo



RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kusitisha utekelezaji wa utaratibu mpya wa tozo za huduma za kibenki ili kuwapa wananchi nafuu ya maisha.

Takwa hilo limetolewa leo katika tamko la chama hicho kwa umma lililotolewa na Naibu wa Sekta ya Fedha na Uchumi, Juma Kombo likiwa na mapendekezi matatu.

ACT Wazalendo kimeitaka pia Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato kwa kuzingatia utajiri wa nchi ukiwemo wa madini, ardhi, bahari, misitu na shughuli za biashara za ndani na nje ya nchi na pia itumie vyanzo vya uzalishaji mali kupata kodi kuliko mifumo ya huduma.

Katika tamko lake hilo, chama hicho kimeitaka Serikali iwe inawashirikisha wanaoguswa na maamuzi yoyote ili kujenga uhalali wa uamuzi wowote inaochukua na kwamba isipuuze vilio wa wananchi kwa kisingizio cha aina yoyote kwa sababu athari zitakazotokana na kulazimisha utekelezaji wa kanuni za tozo hizo mpya zinazowabebesha mzigo mkubwa wananchi ni kubwa kuliko malengo ya kifedha yanayotarajiwa kuvunwa na Serikali.

“Serikali iwafute machozi wananchi kwa kusitisha kabisa na pengo lake lifidiwe kwenye vyanzo vingine ambavyo havitaleta athari,” linaeleza tamko hilo.

Akizungumzia msingi wa kutolewa kwa tamko hilo, Kombo anaandika kuwa Julai, 2022 Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ilitangaza kwenye gazeti la Serikali namba 478V, kuanza utekelezaji wa tozo ya mialama ya fedha kupitia benki.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba


“Utekelezaji wake ulianza papo hapo ambapo tumeshuhudia watumiaji wa huduma za kibenki wanapotoa fedha kwenye ATMs, kaunta kupitia wakala wa benki na huduma za benki kupitia simu za mkononi, wamekuwa wakikatwa kwa viwango tofauti tofauti.

“Makato haya yameongeza mzigo mzito kwa watumiaji wa huduma za kibenki, itakumbukwa mwaka jana Serikali ilianzisha tozo kwenye miamala ya simu, wananchi walilalamikia sana kodi hiyo mpya na kusababisha kupunguza matumizi ya huduma za kifedha kwa chini ya wastani wa asilimia 25.

“Badala ya Serikali kutafuta namna ya kumpunguzia mwananchi mzigo imeendelea kuanzisha kodi mpya kwa watumiaji wa huduma za kibenki. Kuanzishwa kwa tozo mpya kwenye huduma za kibenki kumeibua hisia nzito kwa watumiaji wa huduma hizi kila kona ya nchi, wananchi wanalia kutokana na maumivu yaliyopandikizwa na tozo hizo,” linaeleza tamko.

Aidha, tamko linaeleza zaidi kuwa ACT Wazalendo inaungana na wananchi kupinga utekelezaji wa utaratibu wa tozo hiyo kwa sababu inakata zaidi ya mara mbili kwenye chanzo kimoja na kwamba ni utaratibu usiokubalika kwenye mchakato wa kuanzisha chanzo cha mapato ya Serikali.

Linataja sababu zingine kuipinga tozo hiyo kuwa itashusha ari na hamasa ya wananchi kutumia mifumo rasmi ya kifedha jambo ambalo linaenda kinyume na jitihada zilizofanywa nyuma za kuwaunganisha wananchi kwenye mifumo hiyo.

“Tozo hizi zitapunguza mzunguko wa fedha katika mifumo ya kibenki, wananchi watapunguza kutumia huduma za kibenki ili kukwepa makato yasiyo ya haki kama tulivyoshuhudia mwaka wa fedha 2021/22, Serikali ilipoanzisha tozo kwenye miamala ya simu za mkononi ambapo kulikuwa na anguko hadi kufikia  asilimia 25.6 pekee ya makusanyo sababu ya tozo.

“Tozo zitaongeza ugumu wa maisha kwa kila mtu, awe mfanyabiashara, mkulima, mama lishe au mvuvi na zitakuwa kikwazo katika uchumi wa kidijitali na kurejesha utamaduni wa kuhifadhi fedha nyumbani ambao unaweza kurejesha uvamizi na uhalifu,” linaeleza.

  

.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya