Wednesday, December 25, 2024
spot_img

CHICCO YATEKELEZA AGIZO LA KAFULILA

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Simiyu, David Kafulila (mwenye koti jeuzi) akiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mkoa huo wakikagua ujenzi wa barabara ya Mwingumbi hadi Maswa, hivi katibuni (Picha cha hisani ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

  

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

Kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya CHICCO inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Mwigumbi hadi Maswa, yenye urefu wa kilomita 57 ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo.

Chicco, Kampuni kutoka China inarudia kujenga upya barabara hiyo baada ya kuagizwa na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Simiyu, David Kafulila kurudia kuijenga baada ya kuikagua na kubaini kuwa ilijengwa chini ya kiwango.

Kampuni hiyo ilianza kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 75 mwaka 2018 lakini ilikumbana na rungu la RC Kafulila mwaka 2021, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwasili kwake mkoani Simiyu kama mwakilishi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kumuagiza mkandarasi arudie kuijenga upya baada ya kuigua na kutoridhishwa na kiwango chake cha ubora.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog jana, Kafulila ambaye aliishushia rungu Chicco wiki moja tu baada ya kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Juni 5, 2021 alisema kazi iliyofanywa na kampuni hiyo kwa sasa, ikiwa ni mwaka mmoja tangu alipotoa agizo la kutaka ujenzi huo urudiwe upya, inaridhisha na kwamba utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 96.

“Nakumbuka ilikuwa ni wiki ya kwanza baada ya kuripoti kama RC hapa Simiyu. Hiyo barabara niliiona wakati nakuja kuripoti Simiyu. Nilifanya ziara na Bodi ya Barabara na kuelekeza marudio ya barabara na kumwelekeza mkandarasi kurudia. Nilimsisitiza barabara yake haitapokewa na Rais Samia Saluhu Hasaan ikiwa chini ya kiwango.

“Mbali ya kurudia barabara, pia mshauri mwelekezi (consultant) alibadilishwa, inatia moyo sasa kwani kazi nzuri waliyofanya inaonekana na sasa watu wote wakipita wanafurahi kuona Serikali itapokea barabara imara sawa na thamani ya fedha..

“Huu ni ujumbe wangu kwa wakandarasi wote, hakuna mradi utakaopokewa ukiwa chini ya kiwango ndani ya mkoa wetu wa Simiyu. Kwa sasa nina amani hata Rais akipita kukagua, nina amani kwamba fedha iliyoletwa ndani ya mkoa wetu kwa ajili ya barabara na hata miradi mingine thamani ya pesa inaonekana.. wakandaŕasi wababaishaji hawana nafasi…nimeshavunja na nitaendelea kuvunja mikataba na kila mbabaishaji aliyepata mradi kwa bahati mbaya katika Mkoa wa Simiyu.

“Serikali inalaza mabilioni ya fedha barabarani. Ndio maana lazima kuhakikisha tunabanana. Yaani gharama ya kilomita moja ya barabara ya lami ni takribani Shilingi bilioni 1.5, pesa ambazo zinatosha kukamilisha majengo ya kituo cha afya.

“Sasa upewe mabilioni yote hayo na bado ukabidhi barabara ambayo baada ya mwaka tu imeharibika na kuhitaji mabilioni mengine ya ukarabati? Huu ubabaishaji hauwezi kupewa nafasi ndani ya awamu ya sita. Na kwa upande wetu tutatimiza kipande chetu Simiyu,” alisema.

PANORAMA Blog imemtafuta Meneja wa Tanroad, Mkoa wa Simiyu, John Mkumbo kuzungumzia mwenendo wa utekelezaji wa ujenzi huo ambaye katika majibu yake mafupi alisema kazi inaendelea vizuri na utekelezaji umefikia asilimia kubwa.

“Ninachoweza kusema, kazi ya ujenzi wa barabara hiyo inaendelea vizuri, utekelezaji umefikia asilimia kubwa. Ungekuwa Simiyu ungekuja tukaongea vizuri lakini kama upo Dar es Salaam, siwezi kuongea zaidi ya hayo kwenye simu na ninapigiwa simu na watu wengi sana kuhusu hiyo barabara. Jibu ni hilo, kazi inaendelea vizuri,” alisema Mkumbo..

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya