Monday, June 23, 2025
spot_img

WAZIRI AWATAKA UHAMIAJI KUIMARISHA USALAMA MIPAKANI

MWANDISHI MAALUMU

LOLIONDO.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Hamad Yusufu Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria za nchi.

Waziri Masauni aliyasema hayo mapema wiki hii akiwa Ngorongoro mkoani Arusha alikokwenda  kukagua maendeleo ya kazi ya uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.

Aidha, Masauni alibainisha kuwa Serikali itafanya uhakiki wa kina kubaini uendeshaji wa asasi za kiraia nchini kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na zile zitakazokiuka zitachukuliwa hatua kali za kisheria.

Masauni alieleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya kazi na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, alimueleza Waziri Masauni kuwa amepokea maelekezo yake na atahakikisha hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa wilayani Ngorongoro na kuwa kazi  hiyo itaendelea kwa hali ya amani  na utulivu.



 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya