![]() |
IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Loliondo mapema wiki hii |
MWANDISHI WETU
LOLIONDO
MKUU wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC) John Mongella wamefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kukagua kazi ya kuweka alama za mipaka.
Viongozi hao walifanya ziara hiyo mapema wiki hii na kueleza kuwa wameridhishwa na mwenendo wa kazi wa kuweka alama hizo za mipaka.
Akizungumza baada ya ukaguzi, IGP Sirro awalitaka wataalamun wanaofanya kazi hiyo kujituma ili ikamilike kwa wakati.
Aidha Sirro alitoa rai kwa wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na Serikali kwa sababu la kuweka mipaka hiyo ni kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.
‘Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa’, alisema IGP Sirro.
Kwa upande wake RC Mongella alimhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa kazi inaendeshwa kwa hali ya utulivu na kwa kuzingatia sheria za nchi.
MATUKIO MENGINE KATIKA PICHA IGP SIRRO NA RC MONGELLA WALIPOZURU LOLIONDO