Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro jana aliongoza maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwafunda vijana kuhusu umuhimu wa umoja katika kongamano la vijana Mkoa wa Singida. DC Muro alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Binilith MahengeÂ
Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano ya Chuo cha Uhasibu Singida ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo umuhimu wa kudumisha Muungano, fursa za uchumi katika Mkoa wa Singida na ushiriki wa vijana katika sensa ya watu na makaziÂ
Akizungumza katika kongamano hilo DC Muro alisema Tanzania Bara haiwezi kuwa salama kama Tanzania Zanzibar haitakuwa salama kiulinzi, kiuchumi na kijamiiÂ
Alisema wakati dunia ikiungana katika muktadha mbalimbali ni vizuri kwa Tanzania kudumisha Muungano ili kutoa nguvu ya kuleta maendeleo kwa jamii za pande zote mbili