Monday, June 23, 2025
spot_img

WAANDISHI 8 WASHINDA KESI CMA, KULIPWA SH. MIL 52.8

 


 

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

TUME ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)  imeimpa siku 14 Kampuni ya Ador Tanzania Limited inayochapisha magazeti ya Jamvi la Habari, Times Observer na Jamvi Online Tv kuwalipa Shilingi Mil 53.8 waandishi wa habari wanane waliokuwa wakifanya kazi katika magazeti hayo.

Malipo hayo ni malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuwaondoa kazini bila kufuata utaratibu.

Hukumu hiyo ya usuluhishi ni ya kesi namba  CMA/DSM/KIN/272/2021 iliyofunguliwa Agosti 2021 na ilitolewa Machi 3 mwaka huu na msuluhishi Jaji Kabelinde.

Akisoma hukumu, Jaji Kabelinde alisema baraza lake limejiridhisha kuwa walalamikaji walikuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Ador Tanzania Limited ambao waliajiriwa tarehe na mwaka tofauti tofauti lakini kwa pamoja waliachishwa kazi kwa mdomo Julai 4, 2021 kinyume na sheria.

Katika shauri hilo, walalamikaji nane wakiongozwa na Michael Mbugi na kuwakilishwa na mwanasheria wa kujitegemea Joakim Joliga, walipinga kuachishwa kazi kinyume na utaratibu na kuiomba CMA kumuamuru mlalamikiwa, Kampuni ya Ador Tanzania Limited kuwalipa mishahara waliyokuwa wakiidai, notisi ya kuachishwa kazi, fedha za likizo, kiinua mgongo, malipo ya kufanya kazi saa za ziada, fidia ya kuachishwa kazi na kupatiwa hati ya utumishi.

CMA ilisikiliza shauri hilo upande mmoja  na kutoa hukumu baada ya mlalamikiwa kutofika kwenye shauri licha ya kupelekewa hati ya wito, Oktoba 6, 2021 iliyomtaka mlalamikiwa huyo kufika mbele ya tume Oktoba 21, 2021.

Hati ya kuitwa kwenye shauri ilikuwa na uthibitisho wa Serikali ya Mtaa ya Vigaeni uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa hukumu, shauri lilisikilizwa upande mmoja kwa mujibu wa kifungu cha 87(3)(b) cha Employment and Labour Relations Act no. 6/2004 CAP 366,R.E 2019 ambacho husomwa sambamba na kanuni ya 14(2)(a)(ii) ya GN 67/2007.

Hata hivyo, walalamikaji wameieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa hadi sasa mmiliki wa Kampuni ya Ador Tanzania Limited, Habib Mchange hajaipokea hukumu kama utaratibu wa kisheria unavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kugonga muhuri ili kuthibitisha kuwa imepokelewa.


Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya