Monday, June 23, 2025
spot_img

WANAOTAKA KUHAMA NGORONGORO KWA HIARI WAJITOKEZE – MAJALIWA

 

Waziri Mkuu, Kassin Majaliwa

*Awataka wakajiandikishe kwa DC, asema Serikali itawahudumia

RIPOTA WA WAZIRI MKUU   

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha wanaotaka kuhama kwa hiari yao wajitokeze waseme wanataka kwenda wapi.

“Suala la idadi ya watu ni kubwa. Kumbe huko nyuma kulishakuwa na mapendekezo. Yeyote anayeona anaweza kuishi mahali pengine yuko huru kusema. Kama yuko mtu wa aina hiyo, awe huru kwenda kwa DC (Mkuu wa Wilaya) kajiandikishe na Serikali itakuhudumia vizuri.

“Hayo ni maamuzi ya mtu binafsi, kusiwe na mtu wa kumshinikiza fulani asifanye maamuzi yake. Kama yuko aachwe afanye maamuzi yake, aseme anataka kwenda wapi na sisi tutamhudumia.”

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa kauli hiyo Alhamisi wiki hii alipokuwa akizungumza na viongozi na wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro kwenye kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya zamani ya NCAA, wilayani Ngorongoro. 

Ngorongoro

 

Alisema hata katika suala la ushoroba wa kilometa za mraba 1,500 kule Loliondo kumekuwa na ubishi wa muda mrefu juu ya eneo tajwa lakini hakuna anayejua mipaka halisi ya eneo hilo.

“Ubishi ubishi wa eneo kwenye namba upo kati ya wenyeji na wahifadhi lakini hakuna anayejua kiuhalisia eneo linaanzia wapi na linaishia wapi.

“Haya ni maamuzi ya mwaka 2018 yaliyofikiwa kwenye kikao cha Ololosokwan. Ni vema tukaweka alama za kudumu ili iwe rahisi kubaini eneo hilo; kilometa za mraba 1,500 zijulikane zina ukubwa gani na zinagusa eneo lipi.

“Hakuna jambo linataka kufanywa kwa trick kwa kutaka kumuathiri Mtanzania, hakuna Serikali ya namna hiyo. Kila jambo linalozungumzwa kwenu ni jema tu, linafanywa kwa nia njema,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu ameziagiza mamlaka zote zinazoshughulikia suala la uwekaji wa alama hizo zihakikishe zinawashirikisha viongozi wa maeneo hayo katika hatua zote.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri wa Maliasilna Utalii, Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Naibu Waziri wa Ardhi, Makatibu Wakuu wa wizara za Maji na TAMISEMI na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wadau wengine walioshiriki mkutano huo ni Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai, viongozi wa kimila (Malaigwanan), wenyeviti wa vijiji na vitongoji, Baraza la Wafugaji la Ngorongoro na viongozi wa dini.

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya