Tuesday, June 24, 2025
spot_img

ASA AACHIA NGOMA MPYA ‘MAYANA’

JOSEPH SHALUWA

MWANAMUZIKI  mahiri kutoka nchini Nigeria, ASA ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitafuta njia ya kuutangaza muziki wake kimataifa kwa namna ya kipekee, ameachia ngoma mpya aliyoipa jina la Mayana ikiwa ni pamoja na video yake.

Katika ngoma hiyo iliyotayarishwa na Prodyuza Priime wa Nigeria, ikiwa na mchanganyiko wa Pop, Afrobeat, R&B na Soul, mwanadada ASA ameimba kuhusu maisha ya ndoa huku midundo ya wimbo huo ikiwa na uwezo wa kuchezeka kwenye shughuli mbalimbali za kiburudani hususan kwa watu weusi.

Video ya wimbo huo iliyoandaliwa na Meji Alabi, inadhihirisha hilo kutokana na ubora wake kuanzia picha, mandhari, rangi, fasheni za mavazi na kadhalika, vitu ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa utambulisho wa mtu mweusi kote duniani.

TAZAMA “MAYANA” VISUAL HERE

Akizungumzia wimbo huo, ASA amesema: “Siku zote ninapoandika mashairi ya wimbo mpya, huwa najaribu pia kutengeneza midundo ya hapa na pale inayoendana na mashairi hayo na hapo ndipo wazo la Mayana lilipokuja. Nilikuwa najaribu kumuimbia mtu huyu na nilipoangalia Google, ndipo nilipogundua kwamba kumbe Mayana inamaanisha mponyaji wa kesho.

Ngoma ya Mayana inatoka katika albamu ya tano ya msanii huyo inayotarajiwa kutoka hivi karibuni, ambayo wazo lake alilipata mara baada ya kurejea nchini Nigeria kutoka Ulaya.

Anaeleza kwamba ziara zake za kimuziki barani Ulaya zilisimama kutokana na maambukizi ya Corona na hapo ndipo alipopata wazo la kuandaa albamu hiyo ambayo itasheheni nyimbo nzuri zitakazopendwa na kila mmoja na anatarajia kuizindua albamu hiyo Mei 3, 2022 jijini London katika Ukumbi wa Royal Albert Hall.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya