Wednesday, March 12, 2025
spot_img

CHEMAF SPRL WATAPATAPA

 

Emmanuel Kibwana

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

KAMPUNI ya CHEMAF SPRL sasa imeanza kutapatapa baada ya kuripotiwa kwa habari kuwa imemtelekeza aliyekuwa mfanyakazi wake, Emmanuel Kibwana baada ya kupata ulemavu wa jicho moja akiwa kazini na kutajwa kwa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (TRH) kwenye habari hiyo.

Katika kutapatapa huko, mwanasheria wa kampuni hiyo, Mashaka Ngole jana alipiga simu ya vitisho kwa Tanzania PANORAMA Blog na kukana yale aliyopata kuyaongea pasipokujua kuwa mawasiliano yake na Tanzania PANORAMA Blog pamoja na ushahidi wa mawasialiano ambayo amekuwa akiyafanya na Kibwana anayelalamika kulaghaiwa na CHEMAF SPRL baada ya kupofuka jicho ili aache kazi, yametunza mahali salama.

Kibwana anaituhumu CHEMAF SPRL kutomlipa stahili zake ikiwemo mafao ya pensheni, malipo ya likizo kazini kwa zaidi ya miaka 10 aliyofanya kazi katika kampuni hiyo na fidia ya kuumia kazini na; pamoja naye wafanyakazi wenzake zaidi ya 10 nao wana madai yanayoendena na yake dhidi ya kampuni hiyo.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog jana, Mashaka alihoji kwanini habari hiyo imeandikwa pasipo kampuni anayoitumikia kupewa nafasi ya kuzungumza na kwamba anajiandsaa kukimbilia mahakamani kudai fidia na kuchukua hatua zaidi za kuhakikisha habari hiyo haiendelei kuripotiwa.

Tanzania PANORAMA Blog ilikaribisha hatua hiyo ya Mashaka kwa kumkumbusha kuwa amepata kuwasiliana nayo kuhusu suala la Kibwana na ilimtaka aharakishe kuchukua hatua anazokusudia kwa sababu yeye binafsi na pia kampuni anayoitumikia wanayo haki ya kuchukua hatua za aina hiyo iwapo wataona hakuwatendewa haki katika habari yoyote inayoripotiwa na chombo cha habari dhidi yao.

Rekedi zilizopo Tanzania PANORAMA Blog ambazo zinaweza kutolewa mahali popote zitakapohitajika zinaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza, Mashaka aliwasiliana nayo Oktoba 23, 2021 kupitia simu yake ya kiganjani na kuulizwa kuhusu malalamiko ya Kibwana ambapo pamoja na maelezo yake mengine alishindwa kujibu kuhusu kampuni hiyo kutowasilisha kwenye mifuko ya kijamii makato ya pensheni, mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na fidia aliyopaswa kulipwa Kibwana baada ya kuumia akiwa kazini.

Mashaka aliitaka Tanzania PANORAMA Blog kwenda kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kuulizia kuhusu pensheni ya Kibwana, kwenda WCF kuulizia kuhusu malipo ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na kwamba malipo yote ya fidia kwa Kibwana baada ya kuumia akiwa kazini alikwishalipwa.

Wakati Mashaka akijibu hivyo, nyaraka ambazo Tanzania PANORAMA Blog imeziona zinaonyesha kuwa Kibwana hajalipwa malipo ya fidia ya kuumia kazini, na yheye pamoja na wafanyakazi wenzake zaidi ya kumi, kampuni ilikuwa haiwasilishwi kwenye mifuko ya kijamii fedha za pensheni zao.

Mbali na Mashaka, Tanzania PANORAMA Blog alifika katika ofisi za Tanzania Road Haulage (TRH) Oktoba 26, 2021 kuuliza kuhusu hilo lakini mlinzi mwanamke aliyekuwa getini aliizuia kuingia ndani kwa maelezo kuwa wanaopaswa kulizungumzia suala la Kibwana, wote hawapo ofisini na hata alipoombwa kufanya mawasiliano nao kuhusu uwepo wa waandishi ofisini hapo alisema ruhusa ya waandishi kufika eneo hilo haipo.

Mlinzi huyo aliomba kuonyeshwa picha ya Kibwana ili aone alivyoumia na alipoonyeshwa alisema hamfahamu na kuanza kuwaita walinzi wenzake waiangalie picha hiyo ambapo walimtambua na kueleza kuwa ni kweli alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo. Ili kutoa nafasi zaidi kwa kampuni hiyo kuzungumzia tuhuma na malalamiko inayoelekezewa, mlinzi aliachiwa kadi mbili zenye nambari za simu za Tanzania PANORAMA Blog ili awapatie mabosi kama alivyotaka kwa ahadi kuwa atawapatia ili wapige kutoa ufafanuzi lakini hawakufanya mawasiliano yoyote.

Mwingine aliyezungumza na Tanzania PANORAMA Blog Oktoba 23, 2021 kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu hilo ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya CHEMAF SPR, Mustafa Nanji ambaye alikiri kuwa ni kweli kampuni yake ilikuwa haiwasilishi makato ya pensheni za wafanyakazi wake kwa sababu wafanyakazi hao walikuwa wanakataa kukatwa makato hayo.

Kuhusu WCF na malipo ya fidia ya kuumia kazini kwa Kibwana, Mustafa alitaka aulizwe mwanasheria Mashaka na alituma namba yake ya simu. Ujumbe wenye namba ya simu aliyotuma umehifadhiwa mahali salama.

Tanzania PANORAMA Blog itaendelea kuripoti suala hili pasipo kukiuka miiko, kanuni na taratibu za uanahabari.

 

 

 

 

  

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya