Wednesday, March 12, 2025
spot_img

NIMEPOFUKA JICHO KAZINI, CHEMAF WAMENILAGHAI, WAMENIPIGA TEKE

 

Emmanuel Kibwana

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

EMMANUEL Kibwana, aliyekuwa ameajiriwa na Kampuni ya Chemaf SPRL kama dreva amejitokeza hadharani kueleza jinsi alivyoumia jicho akiwa kazini kisha akalaghaiwa na mwajiri wake, akatelekezwa.

Kibwana alifanya mahojiano na Tanzania PANORANA Blog wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuhusu alivyolaghaiwa na waajiri wake baada ya kuumia jicho ambalo sasa limepofuka, kuondolewa kazini na kunyimwa haki zake.

Alisema alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka kumi lakini alipoumia jicho, aliitwa na maafisa wa kampuni ya Tanzania Road Haulage (TRH) ambao wanasimamia shughuli nyingi za Chemaf, wakamshawishi akubali kuacha kazi kwa hiari kutokana na hali yake ya ulemavu huku wakiahidi kumlipa stahiki zake zote.

“Ninashukuru nimekutana na nyie, sipo vizuri sana lakini naweza kuzungumza kidogo. Nataka mnisaidie kama mnavyosaidia wengine walau nipate haki zangu.

“Mimi nimewafanyia kazi hawa Chemaf kwa zaidi ya kumi, nilikuwa dreva na mara nyingi nilikuwa nasafiri nje ya nchi kupeleka mizigo. Hii Chamef ipo ndani ya TRH kwa sababu mambo yao huko kwenye usajili hayajakaa sawa sana sasa nilipoumia wakaja maafisa wa TRH wakanishawishi kuwa kwa sababu nimekuwa mlemavu tena wa jicho bora njipumzike.

“Walianiahidi kuwa nitalipwa haki zangu zote ikiwemo NSSF na fidia ya kuumia kazini, nikaona ni kweli kwa sababu niliumia sana bora nipumzike. Nikaacha kazi lakini hawakunilipa kabisa, nimejiuguza mwenyewe kwa shida ndiyo sasa nipo kama hivi.

“Wana mafao yangu za zaidi ya miaka kumi kazini hawajanipa, wana sheria wao ndiyo wanamtumia kwenye haya mambo. Huyo muulizeni kwanini sisi watanzania wenzake anashiriki kututendea hivi,” alisema Kibwana kabla hajashindwa kueleza zaiidi kutokana na jicho lake kutoa maji mengi na kulalamika kuwa anasikia maumivu makali.

Tanzania PANORAMA Blog imefika ofisi ya TRH, kurasini, Dar es Salaam, mahali zilipo ofisi za Chemaf ili kupata ukweli wa malalamiko haya lakini ilizuiliwa getini.

Mlinzi wa mlangoni aliuliza sababu za kufuatilia suala hilo, aliomba kuonyeshwa picha ya Kibwana kisha akasema ruhusa ya kufanya mahojiano na kiongozi yoyote kuhusu suala hilo ni lazima itoke utawala na baada ya kupiga simu utawala alisema wahusika wote wanaoweza kulizungumzia  hawapo na hajui watapatikana lini.

Tanzania PANORAMA inaendelea kufuatilia suala hili.   

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya