![]() |
Akif Kara, anayetuhumiwa kulangua umeme na kufanya biashara ya kuuza umeme bila kuwa la leseni ya EWURA |
RIPOTA PANORAMA
0711 46 49 84
MFANYABIASHARA anayetuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ulanguzi wa umeme Akif Kara, ameanza kuweweseka.
Akif, mfanyabiashara anayemiliki Kampuni ya Mar Kim Chemicals ameanza kuweweseka baada ya habari zake kuripotiwa na PANORAMA Blog kuwa anauza umeme kwa bei ya juu na anafanya biashara hiyo bila kuwa na leseni ya EWURA.
Mpaka sasa, Tanzania PANORAMA Blog imebaini Akif kufanya biashara hiyo katika jengo analolimiki kwa ubia na mfanyabiashara Ugur Gurses, lililopo Mtaa wa Livingstone, Kariakoo mkoani Dar es Salaam.
![]() |
Jengo linalomilikiwa kwa ubia kati ua Akif Kara na Ugur Gurses ambalo wakazi wake wanalalamika kulanguliwa umeme |
Wawili hao wanadaiwa kukusanya fedha nyingi kwa lufanya biashara isiyo halali huku Ugur akifikia hatua za kukaidi maelekezo ya EWURA ya kuacha kuvunja sheria.
Jana, baada ya Tanzania PANORAMA Blog kuripoti taarifa za Kara kulangua umeme na kufanya biashara hiyo bila kuwa na leseni ya EWURA, Kara alipiga simu na kuanza kulaumu kuwa kwanini taarifa zake zimeripotiwa.
Kara alitishia kuwa yeye anaongea na maofisa wa juu wa polisi hivyo atawafahamisha ili wawakamate waandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na alipoambiwa aharakishe kufanya hivyo aliomba habari zinazomuhusisha na vitendo vya ulanguzi wa umeme zifutwe.
Tanzania PANORAMA Blog ilimwambia Kara kuwa anao uhuru wa kulalamika kwa namlaka za kisheria au kufungua kesi mahakamani kama anaona habari zake zimeripotiwa kiupotoshaji lakini yeye alisisitiza zifutwe haraka vinginevyo atawafahamisha polisi.
Alipoulizwa iwapo hauzi umeme kwa bei juu na iwapo anayo leseni ya EWURA inayomruhusu kuuza umeme alisema jambo hilo amekwishamwagiza mwanasheria wake kulizunguzia
Kara alielezwa kuwa mwanasheria wake anayefahamika kwa jina la Albert Kimaro amekwishalizunguzia kwa kueleza kuwa ni kweli alikuwa akifanya biashara hiyo kinyume cha sheeria lakini kuanzia mwezi huu amemwelekeza kushusha bei kulingana na bei elekeze ya EWURA, alisema atapambana.
Muda mfupi baada ya Kara kuongea na Tanzania PANORAMA Blog, Albert Kimaro, msemaji na mwanasheria wa Kara naye alipiga simu na kutoa vitisho huku akishinikiza habari hiyo ifutwe.
Kimaro alisema habari hiyo siyo nzuri kwa boss wake na isipofutwa atakwenda mahakamani.
Alipoulizwa kama kuna neno lililopotoshwa kati ya aliyoieleza Tanzania PANORAMA Blog alipokutana nayo juzi, katika Jengo la Posta, Dar es Salaam alisema aliomba iwekwe vizuri lakini anashangaa kila kitu kimewekwa wazi.
Kimaro alikutana na Tanzania PANORAMA Blog juzi, akimuwakilisha Kara aliyemtaka kuja kujibu tuhuma anazoelekezewa za kulangua umeme na kuuza bila kuwa na leseni ya EWURA.
Katika majibu yake alisema ni kweli Kara alikuwa akiuza umeme kwa bei ya juu lakini amemwambia afuate bei za EWURA na kwamba hilo limeishaanza kutekelezwa tangu alipompa maelekezo hayo.
Katika siku za karibuni, Kara anayedaiwa kuvuna mamilioni ya pesa kwa kufanya biashara hiyo alishusha bei ya umeme kwa watu wanaoishi na kufanya biashara katika jengo lake hadi kufikia sh 350 kwa uniti moja kinyume na bei elekezi ya EWURA ambayo ni sh. 292 kwa uniti moja.
Mbia mwenzake, Ugur Gurses yeye alishusha bei ya uniti moja kutoka sh 650 hadi sh 500 huku akikaidi maelekezo ya EWURA ambayo ililifikisha shauri lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua za kisheria.
Tanzania PANORAMA Blog imewasiliana na DPP na itaripoti kauli yake kuhusu suala hili.