Friday, March 14, 2025
spot_img

KANYANI AANZA KUJIBU TUHUMA ANAZOELEKEZEWA

Salim Kanyani

 

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

SALIM Kanyani anayetajwa kuwa mganga wa kienyeji aliyejipatia fedha nyingi kwa njia ya ulaghai ameanza kujibu tuhuma anazoelekezewa.

Kanyani ameiambia Tanzania PANORAMA Blog hivi karibuni kwa njia ya simu kuwa yeye siyo mganga wa kienyeji kama inavyodaiwa na mfanyabiashara Remoy Kibombe, bali alikuwa akimsaidia kufuata dawa za kienyeji kwa waganga sehemu mbalimbali za mikoa ya kanda ya ziwa.

Amesema, mbali na kumsaidia kufuata dawa kwa waganga wa kienyeji pia alimuokoa kutoka kwenye mikono ya matapeli waliokuwa wakila hela zake kwa kumdanganya kuwa watamtafutia dawa za matatizo yake.

“Mimi sipo Dar es Salaam lakini nitakuja kuwaeleza vizuri kuhusu hilo suala. Mwanzo sikuweza kuongea na nyie vizuri kwa sababu sikuamini kuwa ninyi ni waandishi wa habari kweli lakini baada ya kusoma taarifa zenu nimeamini na nawaahidi nitakuja kuzungumza na nyie mjue ukweli.

“Kwa sasa ninachoweza kusema ni kwamba mimi siyo mganga wa kienyeji ila ninawafahamu waganga wengi. Kibombe nilikuwa namsaidia kufuata dawa kwa waganga wa kienyeji sehemu mbalimbali za mikoa ya kanda ya ziwa.

“Nadhani unajua kuwa dawa za kienyeji hazina bei rasmi, ni maelewano hivyo mimi nilikuwa nampa bei waliyokuwa wanasema hao waganga kama ni milioni sita au kumi ananipa namfuata dawa na hilo sidhani kama ni kosa.

“Huyo Kibombe nilimkuta anaendeshwa vibaya na wajanja fulani ambao walikuwa wanamlia hela zake nyingi sana. Mimi ndiyo nilimsaidia sasa nashangaa anasema nimemtapeli zaidi ya bilioni. Hivi ningekuwa na zaidi ya bilioni ningekuwa hivi kweli,” alisema Kanyani.

Kanyani ametoa kauli hii baada ya Tanzania PANORAMA Blog kuripoti kuwa amemfilisi Kibombe baada ya kumtaka ampatie Shilingi bilioni 1.4 ili yeye ampatie maboksi yaliyojaa Dola za Marekani ambazo angeziingiza kwenye biashara zake zingeongezeka kimiujiza na hivyo kumpatia utajiri wa haraka zaidi ya ule aliokuwa nao.

  


 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya