Friday, March 14, 2025
spot_img

KAMPUNI YA BAHDELA YAJIWEKA MBALI NA TUHUMA ZA ULANGUZI WA UMEME

 

Risiti ya malipo ya umeme kutoka kwenye mita zinazotengezwa na Kampuni ya Hahdela

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

KAMPUNI inayotengeneza mita za umeme, Bahdela Company Limited iliyopo Dar es Salaam imejiweka mbali na tuhuma za ulanguzi wa umeme na kufanya biashara ya kuuza umeme bila kuwa leseni ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), zinazomuandama mmoja wa wateja wake, Ugur Gurses.

Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa Kampuni ya Bahdela aliyejitambulisha kwa jina la Mbarak Mohamed, alisema Gurses anapaswa kubebe msalaba wake mwenyewe kwa makosa anayoyafanya.

Mohamed, ambaye simu yake imesajiliwa kwa jina la Mbarak Bates, alisema Gurses aliuziwa mita za  umeme za kuweka kwenye jengo lake kama wanavyouziwa wateja wengine lakini kupanga bei ya kuuza umeme kutoka kwenye mita za Bahdela ni jukumu lake mwenyewe.

Jengo linalomilikiwa na Ugur Gurses

 

“Sisi ni watengenezaji wa mita za umeme, hilo ni kweli. Tunatengeneza na kuuza mita za umeme na tunaiuzia hata Serikali lakini tukishauza basi, hatuhusiki kwa namna yoyote na kupanga bei ya kuuza umeme ingawa ni kweli umeme unaouzwa unatoka kwenye mita zetu.

“Huyo Ugur ni mteja kama walivyo wateja wetu wengine, alinunua mita kwetu lakini kupanga bei na kuuza huo umeme hilo ni la kwake, sisi halituhusu. Kama amekutwa akikiuka sheria za nchi basi abebe msalaba wake mwenyewe sisi hatuhusiki kabisa,” alisema.

Wakati Mohamed akieleza hayo, Meneja Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo ameeleza kuwa gharama ya kununua unit moja ya umeme iliyopitishwa na mamlaka yake haitakiwi kuzidi shilingi 292 kwa uniti kwa T1 kwa umeme unaotumika majumbani na kwamba Bahdela wanatakiwa kutoza shilingi 292 kwa uniti moja ya umeme kutoka kwenye mita zake.

Bates alipoulizwa risiti (token) za umeme zinazotolewa na mita za Bahdela zikiwa na bei juu tofauti na bei elekeze iliyopangwa na EWURA zimetengenezwa na kampuni yake au vinginevyo alishindwa kujibu na kusisitiza kuwa Bahdela haihusiki kwa namna yoyote na makosa yanayofanywa na Gurses huku akiomba jina la kampuni yake lisitajwe kwenye sakata hilo na badala yake mwandishi aandike ‘kampuni moja.’

Hayo yanatokea ikiwa tayari EWURA imekwishaeleza kuwa imewasilisha kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) tuhuma zinazomkabili Gurses za kufanya biashara ya umeme kinyume cha sheria na kuuuza kwa bei ya juu.

Meneja Mawasiliano wa EWYRA, Titus Kaguo

 

Akizungumzia hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja Mawasiliano wa EWURA, Kaguo alisema Gurses ana makosa mawili, la kwanza ni kuuza umeme bila kuwa na leseni ya EWURA na kosa la pili ni kuuza umeme kwa bei ya juu na kwamba EWURA baada ya kubaini makosa hayo ilimpelekea karipio la kisheria lakini alikataa kulipokea hivyo ililifikisha shauri hilo kwa DPP ambaye ana nguvu za kisheria na pia ana vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

Gurses, raia wa Uturuki anayemiliki Kampuni ya Adamas Group ikiwa na ofisi zake Karioakoo, Dar es Salaam inayojihusisha na biashara ya nyumba anadaiwa kufanya biashara ya kuuza umeme wa Tanesco kwa bei ya ulanguzi tangu mwaka 2016.

Walalamikaji, Haykal Hassan na Salem Balleith, wanadai kuwa Gurses, mmoja wa wamiliki wa jengo lenye ghorofa 13 lililopo Mtaa wa Livingstone, aliwauzia ghorofa moja kila mmoja katika jengo hilo lakini amewazui kimabavu kutumia umeme kutoka kwenye mita za Tanesco na badala yake anawauzia umeme kwa kutumia mita za Bahdela kwa bei la juu .

Kwamba Gurses anauza uniti moja ya umeme kutoka kwenye mita za Bahdela kwa shilingi 650 na mkazi anayekataa kununua kwa bei hiyo humkatia umeme.

Gurses ambaye alifikiwa na EWURA na kutakiwa kuacha kulangua umeme kwa sababu kitendo hicho ni kukiuka sheria, alikataa maelekezo hayo na anadaiwa kujigamba kuwa EWURA ameikamata mkononi ndiyo maana aliwafukuza maafisa wadogo wa mamlaka hiyo waliokwenda kumtaka aache ulanguzi wa umeme na aidha amekuwa akienda mbali zaidi kwa kudai kuwa yeye ni mwekezaji na ‘mama’ amekwishaagiza wawekezaji wasiguswe kwa lolote kwa sababu anawahitaji sana.

Jitihaza za kumtafuta DPP kuzungumzia shauri hili bado zinaendelea.

   

     

   

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya