Wednesday, June 25, 2025
spot_img

MGANGA WA KIENYEJI ALIYETAJIRIKA KWA UTAPELI

RIPOTA PANORANA

0711 46 49 84

WIKI iliyopita, Tanzania PANORAMA Blog iliandika sehemu ya kwanza ya mkasa wa mfanyabiashara Remoy Kibombe aliyefilisika kwa sababu ya tamaa ya kupata fedha nyingi za haraka haraka baada ya kuhadaiwa na mganga wa kienyeki, Salim Kanyani aliyemweleza kuwa ana majini ambayo yana ‘pesa za majini’ anazoweza kumsaidia kuzipata na kuongeza utajiri wake kwa kiwango akitakacho iwapo atatimiza masharti ya majini hayo.

Ripoti hiyo ilieleza kinaga ubaga jinsi mfanyabiashara Kibombe alivyofahamishwa kwa mganga huyo wa kienyeji na aliyekuwa dalali maarufu jijini Mwanza, Marehemu Hashimu Shimweta aliyefariki baada ya kupondwa na mawe.

Kwamba lengo la Kibombe kwenda kwa mganga Kanyani ilikuwa kutafuta tiba ya matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimkabili na akiwa anapatiwa matibabu ndipo aliposhawishiwa kujipatia maelfu za Dola za Marekani za majini ambazo sharti lake ilikuwa kulipa fedha za kibinadamu, (fedha halisi) jambo ambalo alilitekeleza. Hii ni sehemu ya pili ya ripoti hiyo maalumu.

Miongoni masharti ambayo mganga wa kienyeji Kanyani alimpatia mfanyabiasha Kibombe ayatekeleze ili apate fedha za majini zitakazomuongezea utajiri wake ni kusajili laini ya  simu kwa jina lake kisha amkabidhi na ndiyo awe anamtumia fedha kila anapopata  baada ya kuwa amekwishampatia mkupuo wa kwanza wa fedha alizoelekeza kuwa zinatakiwa na majini yake, Sh. Milioni 600.

Kibombe alitekeleza pia sharti hilo na kuanza kumtumia fedha Kanyani huku akianza kupata upinzani kutoka katika familia yake wa jinsi alivyokuwa akiuza mali na kupeleka fedha kwa mganga huyo.

Akiwa katika utekelezaji wa sharti la kusaka pesa kama alivyoagizwa na Kanyani, mfanyabiashara Kibombe alichukuliwa na mganga huyo na kupelekwa Mkonga, eneo ambalo liko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga yaliko makao makuu ya shughuli za mganga huyo kwa  ajili ya kwenda kufanyiwa tambiko la mizimu na baada ya shughuli hiyo alirejeshwa mkoani Mwanza kuendelea kusaka fedha za kukanilisha malipo aliyotakiwa.

Baada kuwa amekwishalipa zaidi ya Sh bilioni 1.4  alianza kudai apewe Dola za Marekani za majini alizokuwa ameahidiwa na mganga Kanyani bila mafanikio na ndipo alipobaini kuwa alikuwa ametapeliwa na kuanza kutafuta msaada wa vyombo vya ulinzi na usalama ili mganga huyo akamatwe na kufikishwa mahakamini.

Hata hivyo Kibombe alijikuta kwenye wakati mgumu wa utoaji maelezo ya mkasa huo kutokana na kukubaki ghiliba za Kanyani ikiweno kusajili laini ya simu kwa jina lake na kumpatia kisha akawa anatuma fedha kwenye laini hiyo.

Tanzania PANORAMA Blog imebaini kuwa mfanyabiashara Kibombe alijikuta kwenye wakati  mgumu wa kuaminiwa maelezo yake kwa sababu kwa mtizamo wa haraka haraka, madai kuwa alikuwa akimtumia Kanyani fedha kwa simu yanafifia kwa sababu fedha hizo alikuwa akizituma kwenye laini aliyoisajili kwa jina lake hivyo ni rahisi kuaminika kuwa alikuwa akijitumia fedha yeye mwenyewe.

Aidha, Kibombe alijikuta katika hali ya wasiwasi kueleza jinsi alivyoonyeshea maboksi sita yaliyojaa Dola za Marekani ambazo imeelezwa kuwa sasa amekwishabaini kuwa hazikuwa  halisi kwa sababu vyombo vya dola vinaweza kumuunganisha kwenye kosa la matumizi ya Dola za Marekani zisizokuwa halisi.

ITAENDELEA.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya