Wednesday, June 25, 2025
spot_img

KIWANDA CHA BETRI GRAVITA CHAFUKIA KEMIKALI HATARI ARDHINI

 


RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

KIWANDA cha kutengeneza betri za magari cha Gravita kilichopo eneo la ukanda wa viwanda, Misugusugu, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani kimezika ardhini kemikali zenye madhara kwa afya ya udongo na binadamu.
Habari za kuaminika zilizofikia Tanzania PANORAMA Blog kutoka ndani ya kiwanda hicho zimeeleza kuwa kemikali zilizofukiwa ardhini ni zile zilizokwishatumika kutengenezea betri za magari ambazo zinapaswa kuteketezwa na si kuzikwa ardhini. 
 
Watoa taarifa wetu kutoka ndani ya kiwanda hicho wameeleza kuwa kazi ya kuzika ardhini kemikali hiyo hatari hufanyika siku za mwiahoni mwa wiki ambapo wafanyakazi wengi wanakuwa wamepumzika na waliongeza kuwa ni kazi inayofanyika wakati wa usiku tu.
 
Vyanzo zaidi vya habari vya Tanzania PANORAMA Blog kutoka ndani ya kiwanda hicho vimeeleza kuwa kina miubdombinu mizuri iliyopasishwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ya uteketezaji kemikali zinazotumika kwa shughuli za viwandani lakini haitumiki ipasavyo.
 
“Kuna mambo ya hatari sana yanafanyika hapa kiwandani. Hizi betri kuzitengeneza kuna kemikali hutumika na hiyo kemikali inapaswa kuteketezwa kabisa baada ya kutumika.  Hapa kiwandani kuna miundombinu mizuri tu ya uteketezaji wq kemikali hiyo lakini haitumiki ipasavyo kwa sababu hawa jamaa wanakwepa gharama.

“Badala yake wanatumia njia hii ya kufukua mashimo na kuzika hiyo kemikali. Hili eneo likija kuchungzwa litakutwa na kemikali ardhini na ujue madhara yske ni kwamba hii kemikali inasambaa huko ardhini, baada ya muda eneo lote hili litakuwa la ardhi iliyokufa kwa sababu ya kemikali wanayoizika hawa jamaa.

“^Wanachokifanya siku za mwsho wa wiki ambazo wafanyakazi wengi hawaji kazini wao humwambia dreva wa greda kuchimba mashimo ambayo kemikali hiyo huzikwa humo kisha greda hilo hufukia hayo mashimo.

“Vizazi vyetu vitakuja kuishi kwenye eneo lililokufa kwa sababu ya tamaa ya kupata pesa nyingi ya hawa jamaa. Ushahidi kamili upo na wewe tunakupa ili wakibisha tu muutoe. Na hata pakija kupimwa hapa wataalamu watagubdua kemikali nyingi tu inazikwa ardhini,” alisema mtoa taatifa wetu.

Tanzania PANORAMA Blog iliutafuta uongozi wa kiwanda hicho kwa njia ya simu kuzungumzia suala hilo. Katika majibu yake afisa aliyetambulika kwa jina la Goodluck Komba ambaye hata hivyo alikataa kueleza nafasi yake aliomba kukutana na Tanzania PANORAMA Blog ofisini kwake kwa mazungumzo na alipoambiwa lengo la kupigiwa simu siyo kuketi chini kwa mazungumzo bali kujibu maswali aliyoulizwa alilisitiza kuwa anahitaji mazungumzo.

Tanzania PANORAMA Blog itachapisha ripoti maalumu kuhusu kemikali hizo hatari zinavyofukiwa ardhini na kiwanda hicho na madhara yake kwa ardhi na watu wanayoitumia.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya