Wednesday, June 25, 2025
spot_img

WINGU JEUSI BIASHARA YA MABAKI YA MAGAZETI

Mabaki ya magazeti ya nje yanayouzwa hapa nchini

RIPOTA WA PANORAMA

WINGU jeusi limetanda kwenye biashara ya mabaki ya magazeti kutoka nje ya nchi, baada ya mfanyabiashara Said Ali Omar wa jijini Dar es Salaam kubainika kutumia njia za udanganyifu za upokeaji fedha anazokusanya kwa kufanya biashara hiyo.

Omar ambaye pia anatajwa kuwa mfanyabiashara wa maturubai anadaiwa kuwa biashara yake ya magazeti inamuingizia zaidi shilingi milioni 200 kwa nwaka lakini anaficha ukweli huo kwa kutumia akaunti binafsi kupokea fedha xa mauzo za magazeti. 

Taarifa za uhakika zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog zimeonyesha kuwa Omar ni mmiliki wa Kampuni ya Riyal Investment LTD, ofisi zake zikiwa Kariakoo, Dar es Salaam, iliyosajiliwa chini ya kivuli cha ofisi za kampuni nyingine (jina limehifadhiwa) inayojihusisha na biashara ya kununua mabaki ya magazeti ya nje na kuyauza.

Kwamba kwa kutumia kampuni yake hiyo, Omar amekuwa akifanya biashara ya mamilioni ya shilingi lakini sehemu ya mapato yatokanayo na biashara hiyo huyaelekeza kwenye akaunti yake binafsi na kiasi kingine kidogo ndicho hukiingiza kwenye akaunti ya kampuni yake ya Riyal. 

Imeelezwa kuwa Omar anatumia mbinu hiyo kufanya biashara yake ili kukwepa mikono ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na kwamba ili kujificha ukweli wa mapato ya biashara yake amekuwa na utaratibu wa kufungua kampuni ambazo huzitumia kwa muda kisha huzifunga na kufungua nyingine. 

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa kabla ya kufungua kampuni yake ya sasa, Omar alikuwa na kampuni nyingine inayifahamika kwa jina la Sao Mail aliyoifungulia mkoani Mtwara akiwa na ubia na mfanyabiashara mmoja mwanamke ambayo ilifungwa baadaye na kuja kufungua aliyonayo sasa mkoani Dar es Salaam. 

Alipoulizwa kuhusu madai hayo Omar alisema kweli yeye ni mfanyabiashara wa mabaki ya magazeti kutoka nje ya nchi lakini biashara hiyo imesamehewa kodi hivyo haoni sababu ya kuhojiwa kuhusu mwenendo wake kibiashara.

Alipoulizwa ni kwanini amekuwa akitumia akaunti binafsi kuweka fedha za biashara ya magazeti wakati ana akaunti ya kampuni kwa ajili ya biashara hiyo alisema suala hilo amekwishamalizana na TRA bila kueleza zaidi alilimaliza kwa namna gani na maofisa waliohusika kumalizana naye.

Akizungumzia biashara ya maturubai alisena biashara hiyo ameiacha yapata miezi sita sasa na hesabu zake zote zimekaguliwa na TRA na kukutwa zimenyooka.

Hata hivyo uchunguzi wa Tanzania PANORAMA Blog umebaini kuwa Omar analo ghala kubwa la kuhifadhia bidhaa lililo chini ya jengo la ghorofa karibu la makao makuu ya klabu ya Yanga ambalo halifahamiki na mamlaka yoyote kuwa ni mali yake wala bidhaa alizohifadhi humo.

Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa kodi za ndani wa TRA kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa na Tanzania PANORAMA Blog inaendelea kumtafuta ili kulizungumzia.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya