![]() |
Zuchu |
MWANDISHI WA PANORAMA
KAMPUNI kubwa ya muziki ya Apple Music inasherehekea mwezi wa kipekee kwa wasanii wa muziki kwa kuwaunganisha kwenye chati moja, huku msanii wa Tanzania, Zuchu akiwa miongoni mwa mastaa kutoka hapa Afrika Mashariki.
Apple Music imetenga mwezi huu – Mei, ikitumia kaulimbiu ya ‘umoja na ujumbe wa mshikamano’ ikiwa ni mwezi mahususi walioupa jina la Mwezi wa Afrika.
Kampeni hii pia inamulika kizazi kipya cha wasanii wa Afrika wanaobadilisha simulizi katika tasnia ya muziki nyumbani na ng’ambo.
Hiyo inahusisha playlist mahususi ya umoja kwa ajili ya Mwezi wa Afrika inayojumuisha baadhi ya nyimbo bora za kushirikiana barani za hivi karibuni, kukiwa na muziki kutoka kwa Focalistic na Davido, Naira Marley na Busiswa, Gyakie akimshirikisha Omah Lay pamoja na AKA akimshirikisha Burna Boy.
Pia pamejumuishwa playlist 12 ngeni na mahususi kutoka kwa wasanii wakiwemo Omah Lay (Nigeria), Manu Worldstar (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo/Afrika Kusini), Tems (Nigeria) na Amaarae (Ghana), wote wakiwa wamewahi kuhusishwa kwenye mpango wa Apple Music wa kuwaangaza wasanii wanaochipukia, Africa Rising.
Wakiwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza Kireno (Lusophone) wapo Nenny (Cape Verde) na Calema (São Tomé and Príncipe).
Mbali na Zuchu, kutoka Afrika Mashariki, msanii mwingine ni Nviiri The Storyteller (Kenya), kwa nchi za Afrika zinazozungumza Kifaransa (Francophone) kuna Suspect 95 (Ivory Coast) na Tayc (Cameroon), na mwisho wakiwakilisha nchini za Kusini mwa Afrika, Focalistic (Afrika Kusini) na mshindi wa tuzo ya BET Sha Sha (Zimbabwe).
Orodha hizi za kucheza zimeundwa na nyimbo zinazowafanya wasanii wajivunie kuwa Waafrika au ambazo zimebadilisha sura ya muziki wa Afrika.
Mwezi wa Afrika utaungwa mkono pia kupitia Apple Music Radio, Africa Now Radio na Cuppy kitaendesha kipindi kwa ajili ya Mwezi wa Afrika maalum kwa ‘Umoja’ Jumapili ya Mei 30 kusherehekea kutimiza mwaka mmoja ya kipindi hicho na kutoa heshima kwa baadhi ya nyimbo bora za ushirikiano barani.
Kwenye The Ebro Show cha Apple Music 1, kila wiki Ebro atamhoji mgeni kutoka kanda tofauti kuzungumza kuhusiana na playlist yao maalum ya Mwezi wa Afrika pamoja na kuhusisha mchanganyiko wa muziki wenye hamasa (Motivation Mix) kila wiki kutoka kwa Madj maarufu barani Afrika wakicheza nyimbo bora za Amapiano, Afrobeats na zingine.
Sikiliza maudhui yote haya kupitia Apple Music pekee http://apple.co/AfricaMonthUmoja