Thursday, July 17, 2025
spot_img

HAMISI ADAIWA KUGHUSHI SAINI YA KAKA YAKE APATE USIMAMIZI WA MIRATHI

 

Hati yenye jina, saini na picha ya Mtumwa Abud Lukongo inayodaiwa kughushiwa na Hamisi Abud Lukongo na kisha kuitumia mahakamani ili kupewa nguvu za kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Lukongo

MWANDISHI WA PANORAMA

HAMISI Abud Lukongo, anadaiwa kughushi saini ya kaka yake katika hati ya mirathi ili apate haki ya kuwa msimamizi wa mirathi wa familia ya marehemu mzee Lukongo.

Hamisi anatuhumiwa na ndugu zake kuwa alighushi saini ya kaka, Mtumwa Abud Lukongo na kupachika picha yake katika hati ya mirathi kabla ya kuiwasilisha mahakamani akitaka atambulike kuwa amepata ridhaa yake kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Lukongo ambaye ni baba yao.

Mmoja wa wanafamilia ya Lukongo aliyezungumza na Tanzania PANORAMA kwa ombi la jina lake kuhifadhiwa ameeleza kuwa Hamisi ni mdogo wake Mtumwa na alitenda jinai hiyo mwaka 2015 wakati kaka yeye huyo akiwa Ulaya alikokuwa akiendesha shughuli zake.

Pamoja na Hamisi, hati hiyo ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiona imesainiwa siku moja, Agosti 31, 2015 na wanandugu 12 ambao ni Asia Abdu Lukongo, Khadija Abdu Lukongo, Mtumwa Abdu Lukongo, Mwanaasha Abdu Lukongo, Abdulrahman Abdu Lukongo na Mohammed Adub Lukongo.

Wengine waliosaini hati hiyo ni Asha Abdu Lukongo, Mariam Kondo Kilima, Saumu Mohamed, Mwajabu Ally, Hamisi Abdu Lukongo kama mlezi wa Karimu Abdu Likongo na Hanif Issa Ituwa kwa niaba ya Tatu Abdu Lukongo.

“Akiwa Ulaya alikuwa anawasaidia ndugu na wadogo zake kwa sababu ni anajua ni wajibu wake. Merehemu baba yao alikuwa na zaidi ya mke mmoja hivyo Mtumwa alikuwa na wajibu wa kuwaangalia baba yao kufariki.

“Sasa aliporudi nyumbani kutoka nje na kuanza kuangalia mwenendo wa maisha ya wazazi wake waliosalia na baadhi ya ndugu zetu ndipo akagundua kuna tatizo na alipofuatilia akaonyeshwa hati inayomtambulisha mdogo wangu kuwa msimamizi wa mirathi ambayo na yeye kuna saihi na picha yake wakati ile siyo saihi yake kwa sababu ameikana na kweli siyo ya kwake kwa sababu ya kwake inajulikana na hata hivyo wakati hati hiyo inaandaliwa yeye alikuwa nje ya nchi, ile hati ilitengenezwa akiwa hayupo, huyo Hamisi ni mtu hatari sana,” alisema Mtumwa.

Inadaiwa Hamisi alifanikisha mpango wake huo wa kughushi nyaraka kwa msaada wa mmoja wa ndugu zake ambaye ni mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kwamba amekuwa akigawana naye mapato yanayotokana na mali za urithi za marehemu huku ndugu wengine wakifichwa kiasi halisi cha mapato hayo.

Nyuma ya mipango hiyo, anatajwa pia mfanyabiashara Ali Said wa jijini Dar es Salaam kutoa ufadhili wa fedha kuhakikisha hati hiyo ya kughushi inapita mahakamani kwa makubaliano la kupangishwa eneo linalotumika kama ghala ambalo ni mali ya familia ya marehemu Lukongo.

Alipoulizwa Mtumwa kuhusu madai ya saini yake kughushiwa na mdogo wake Hamisi jambo hilo lina ukweku na kwamba limemsikitisha sana lakini alisema atalizungumzia vizuri zaidi baadaye.

Picha ya Hamisi Abud Lukongo iliyopo kwenye hati anayodaiwa kuighushi ili kipata haki ya kuwa msimamizi wa mirathi ya merehemu Lukongo


Naye Hamisi alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema mambo ya familia yao hayapaswi kuingiliwa na vyombo vya habari na akataka kaka yake anayemtuhumu afikishiwe ujumbe kuwa hatafanikiwa bali anapoteza muda wake bure.

Mfanyabiashara Ali alipoulizwa kuhusu uhusika wake kwenye njama hizo alisema anayepaswa kuulizwa ni bosi wake ambaye aliyeingia mkataba na Hamisi wa kukodisha eneo la biashara la familia ya marehemu Lukongo   lakini alikataa kumtaja jina wala kutoa mawasiliano yake.

 

 

 

 

  

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya