Thursday, September 11, 2025
spot_img

TUHUMA ZA UKWAPUAJI MALI ZA MAREHEMU ZAZIDI KUTOKOTA

 

Marehemu Yusuph Dali

MWANDISHI WA PANORAMA

SIKU moja baada ya Dali Yusuph Musa anayedaiwa kujitwalia mali zinazohamishika na zisizohamishika za marehemu Yusuph Dali kwa njia za ulaghai, dada wa marehemu Dali, Mwajuma Zawayai naye amebainika kukwapua mamilioni ya pesa za marehemu Dali.

Mwajuma ambaye tangu juzi alikuwa akikataa kutoa ushirikiano wa kueleza anachokijua kuhusu malipo ya bima ya marehemu Dali anayedaiwa kufariki dunia baada ya kugongwa na gari nchini Italia mwaka 2019, jana ameeleza kuwa bima siyo mirathi ambayo kila mtu ni lazima aipate, ndugu zake aliowapa na wao walisaidiwa mengi na marehemu.

Inadaiwa Marehemu Yusuph Dali, Mtanzania aliyekuwa akijishughulisha na ubaharia alifariki dunia April, 2019 baada ya kugongwa na gari nchini Italia na mwili wake alisafirishwa mwezi mmoja baadaye kurejeshwa nchini na kwenda kuzikwa mkoani Lindi.

Kwamba wakati wa uhai wake, marehemu Dali alimuita Mwajuma kwenda Italia kutafuta maisha lakini walifarakana muda mfupi baadaye kwa sababu marehemu hakupendezwa na aina ya maisha ya dada yake huyo pamoja na magenge aliyokuwa akiandamana nayo hivyo kila mmoja alishika njia yake.

Inadaiwa zaidi kuwa baada ya kifo cha marehemu Dali, Mwajuma ambaye alikuwa bado nchini Italia alihusika katika madai ya bima akiwasaidiwa na watu ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu hawajapatikana kuzungumza na baada ya kukamilisha taratibu muhimu za madai hayo ndipo mwili wa marehemu ulisafirishwa kuja nchini, ikiwa ni mwezi mmoja tangu alipofariki.

Kwamba Mwajuma hakusafiri na mwili wa marehemu kaka yake kutoka Italia kwa ajili ya kuja kuuzika nyumbani bali alibaki huko akipambana kupata malipo ya bima ya kifo cha Yusuph na baada ya kuyapata, alirejea nchini na kuwagawia baadhi ya ndugu huku kiasi kikubwa cha fedha akikitia kibindoni na kuwanyima ndugu wengine.

 Tangu kuibuka kwa madai ya kukwapuliwa kwa malipo hayo ya bima na pia mali za marehemu kuchukuliwa kwa njia zinazodaiwa kuwa za ulaghai, Mwajuma hakuwa tayari kuzungumza lolote lakini jana baada ya kutafutwa kwa njia ya simu kwa muda mrefu, alituma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani ambayo imesajiliwa kwa jina la Rehema Ridhiwani uliosomeka; “kaka naomba uniache, nimefunga mimi nimechoka,”

Tanzania PANORAMA ilimuuliza kwa njia hiyo hiyo ya ujumbe mfupi wa maandish: “kwahiyo unaniruhusu niendelee na story?” na yeye alijibu; “wewe kama umetumwa fanya utakavyojisikia. Hujui sheria za ile nchi fanya unavyoweza,”

Mahojiano hayo mafupi kupitia ujumbe mfupi wa simu yaliendelea hivi;

Mwajuma Zawayai



Tanzania PANOROMA– Nimejieleza vizuri tangu mwanzo lakini bahati mbaya hutaki kuelewa. Sawa nimekubaliana na wewe.

Mwajuma – Na bima siyo mirathi kila mtu apate. Niliowapa ndugu zangu na wao walisaidiwa mengi na marehemu shida iko wapi jamani?”

Tanzania PANORAMA – Kwa hiyo ni kweli kwamba hiyo hela ya bima ulichukua wewe ndiyo ukaja kuwagawia uliowataka wewe?

Mwajuma – Siwezi kupewa mimi, mimi siyo mwanawe. Zaidi ya hayo sitaki kujua nendeni mahakamani. Huyo mtoto wao ndiyo awape mimi ni kama wao tu.

Tanzania PANORAMA – Mbona umesema uliowapa ndugu zako na wao walisaidiwa na marehemu? Maana yake wewe ndiyo uligawa hiyo pesa. Je wewe ndiyo ulikuwa msimamizi wa miradhi?

Mwajuma- Mwanawe. Mimi changu nilichopata nimegawana na wenzangu hao wanaodai wamfuate mwanawe, sio mimi. Mniache.

Tanzania PANORAMA– wewe chako ulipata shilingi ngapi na nani alikugawia?

Mwajuma- Kesi ya miaka miwili mnaleta leo? Nani ana pesa hapa? Wameshindwa kwenye mali ndiyo wananifuatilia mimi? Kwanini wasinifuate mwenyewe  na kuniuliza?  Siwezi kusema na haiwahusu ndiyo maana nasema fanyeni au fuatilia uliyoambiwa huko. Mi usiulize kwanza na njaa sina kitu mniache.

Tanzania PANORAMA – Pole sana kwa njaa dada, Nisaidie hili dogo tu, pesa ya bima ya marehemu iliingia kwenye akaunti ya nani?

Mwajuma –Ukiendelea na huku nakublock, naona umetumwa. Kama askari njoo unikamate tu. Sijui. Kaulize benki zote mi sijui, huo ni ujambazi. Muulize mwanawe.

Tanzania PANORAMA- Hiyo ni hiari yako Mwajuma, ninachofanya ni kukutendea haki ili nisiandike story ya upande mmoja.

Mwajuma– We wasikilize tu. Ukweli hautoki gazetini wao si wamewafahamisha kama ndugu yao? Kwanini hawakunitafuta na kuniuliza wala kujua marehemu yaliyomkuta wanawaza pesa tu. Hata kaburi lake hawana habari nalo walikuwa ndugu wa maslahi siyo wa uchungu, ni aibu kubwa sana. Mimi waongee watakavyo lakini ninatakwenda kwenye vyombo vya sheriau

Tanzania PANORAMA –Dada una haki ya kwenda kwenye vyombo vya sheria wala hakuna anayekuzuia la muhimu kwangu jibu ninachokuuliza.

Mwajuma – Sijui basi. Siyo lazima kujibu. Kwahiyo uniache huru fanya unavyojua.

Tanzania PANORAMA– Sawasawa dada.

Mtaalamu wa masuala ya Bima, ambaye ni Mkurugenzi Mratibu Kanda wa Shirika la Bima Zanzibar, Ali Makame alipoulizwa kuhusu utaratibu unaotumika kutoa na kugawanya fedha ya bima ya kifo amesema, sheria inaelekeza Bima na kifo kulipwa katika akaunti ya mirathi iliyoko Hazina na Hazina ndiyo hugawa fedha hizo kwa warithi. Alisisitiza kuwa utaratibu huo ndiyo unaotumika kwa bima za aina hiyo zinazolipwa nchini au nje ya nchi.

Kabla ya Mwajuma kutoa majibu hayo, Tanzania PANORAMA ilipigiwa simu na mchezaji mpira wa zamani, Iddi Pazi ambaye alijitambulisha kuwa ni kaka wa marehemu na kuhoji kwanini anafuatiliwa na kuonya kuwa iwapo hali hiyo itaendelea asilaumiwe mtu.

Baadaye mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawayai naye aliipigia simu Tanzania PANORAMA Blog akieleza kuwa amefikishiwa malalamiko na dada yake Mwajuma kuwa mtu kuna anafuatilia maisha yake hivyo aingilie kati kumsaidia lakini alijibiwa kuwa anachoulizwa Mwajuma ni maswali mepesi ya kawaida yenye lengo la kumpa nafasi ya kuzungumzia au kutoa ufafanuzi dhidi ya tuhuma na madai anayoelekezewa.

Mwajuma anadaiwa kuwa na msuguano mkubwa na marehemu Dali siku chache kabla ya kufikwa na umauti na kwamba alikusudia kumrejesha kutoka Italia kuja nyumbani Tanzania jambo ambalo Mwajuma hakuafiki.

Aidha, inadaiwa kuwa marehemu Dali aliwasiliana na ndugu yake Juma Abdul akilalamika kwa kudanganywa kuwa ana mtoto wakati hana uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke. Kwamba alibaini hilo baada ya kupata mwanamke wa kizungu aliyemtaka wapime afya zao kabla ya kuoana ndipo akabainika kutokuwa na uwezo huo.

Kwamba marehemu Dali ambaye hapo awali aliagiza kutiwa ndani kwa mtu anayedai kuwa ni mwanaye, Dali Yusuph Musa katika Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama baada ya kutaka kuuza moja ya nyumba zake, aliagiza mali zake zote zirejeshwe baada ya kupata matokeo ya vipimo hivyo akiwa Italia lakini muda mfupi baadaye alifariki kwa ajali ya gari.

 ITAENDELEA

 

 

 

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya