Monday, June 30, 2025
spot_img

JESHI LA POLISI LASAKA FAILI KESI YA KUGHUSHI, UTAPELI MeTL

 

Mmoja wa wakurugenzi wa MeTL. Mohamed Dewji

NA MWANDISHI WETU

JESHi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni bado halijafanikiwa kilipata faili la kesi ya kughushi, lenye nambari RB, WH/IR/2657/2014 ambalo mlalamikiwa ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Murtaza Alihussein Dewji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (RPC), Naibu Kamishna, Ramadhani Kingai, jana ameieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa jitihada za kulitafuta faili la kesi hiyo bado hazifanikiwa lakini zinaendelea na kwamba anaamini hadi leo (Ijumaa) faili hilo litakuwa limepatikana.

“Bado hatujalipata faili la hiyo kesi, bado halijaonekana, bado tunalitafuta.

Ujue kesi hii ni ya siku nyingi na ninashangaa kwa nini huyu mlalamikaji alikuwa amekaa kimya.

“Ni muhmu kumpata mpelelezi wa kesi hiyo kwanza lakini wapelelezi wanabadilishwa kila mara. Sasa tukishamjua mpelelezi, maana anaweza kuwa kwenye kazi nyingine au hayupo hapa kabisa. Lakini tukimpata itakuwa rahisi maana inawezekana faili hilo halijafungwa.

“Ukishakata simu,  nitawauliza watu wangu walipofikia, nitamwita RCO aniambie wamefikia wapi lakini mpaka kesho naamini litakuwa limepatikana,” alisma RPC Kingai.

RPC Kinondoni, Ramadhani Kingai


Wakati RPC Kingai akieleza hayo, uchunguzi wa Tanzania PANORAMA Blog umebaini kuwa jeshi la polisi kupitia kilichokuwa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai, lilitimiza wajibu wake wa kupeleleza kesi hiyo na baada ya kukamilisha upelelezi wake liliuwasilisha kwa mamlaka za juu kwa ajili ya kuchukua hatua.

Habari za uhakika kutoka ndani ya jeshi la polisi pamoja na nyaraka kadhaa za skendo hiyo ambazo Tanzania PANORAMA Blog limeziona, vinaonyesha kuwa Mkurugenzi wa MeTL, Murtaza Dewji alikuwa na nyaraka za kughushi ya makubaliano ya mauziano ya kiwanja namba 105 kilichopo Mbezi eneo la viwanda.

Ripoti ya uchunguzi wa nyaraka hizo inaonyesha kuwa Disemba 5, 2014, jeshi la polisi kupitia kitengo chake cha uchunguzi wa makosa ya jinai, lilitoa ripoti ya majibu ya  uchunguzi wa maandishi na alama uliofanywa na ASP Chrisantus Kitandala, iliyokuwa ikionyesha ubatili wa nyaraka na sahihi zilizodaiwa na Murtaza kuwa ni halali na kwamba alizisaini yeye kwa niana ya MeTL na Ravji Govind Varsani wa niaba ya Kampuni ya Ravji Construction Ltd.

Sehemu ya ripoti hiyo ya uchunguzi wa makachero wa polisi inaeleza kuwa, Agosti 22, 2014 na Novemba 3, 2014 kitengo cha makosa ya jinai makao makuu ya polisi kilipokea nyaraka zilizofungwa kutoka kwa askari mwenye namba E 5497 D/CPL Joash na E 3823 D/SSGT Peres.

Askari hao walieleza kuwa wameagizwa na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Wilaya ya Kipolisi Kawe kuwasilisha nyaraka hizo kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai na nyaraka hizo zilikuwa na kumbukumbu nambari KW/B.1/1/VOL.VII/120 na KW/B.1/1/VOL.1X/35 za tarehe 22 Agosti, 2014.

Kwamba Polisi Kawe waliomba kufanyika uchunguzi wa saini na mihuri katika nyaraka zilizotumwa ili kuweza kubaini ukweli wake.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchunguzi ulifanywa kwenye mkataba wa makubaliano ya mauziano (MOU) kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 1.2 ya kiwanja namba 105 kilichoko Mbezi.

Karatasi au nyaraka saba zilizoelezwa kuandikwa na Ravji Govind Varsani zilifanyiwa uchungizi na pia karatasi au nyaraka tano, moja ikiwa ya mwanasheria kutoka Kampuni ya Bwana Attorney ya Februari 27, 2013, pamoja na saini yake na mihuri anayotumia katika ofisi yake vilifanyiwa uchunguzi,

Sehemu ya ripoti hiyo ya uchunguzi wa makachero wa polisi yenye kurasa 12  na iliyoandikwa kwa lugha ya kimombo inasomeka; “I have examined and compared the disputed signature on exhibit ‘A’ marked ‘X’ together with the specimen signatures on exhibits ‘B1 – B7,  B8 and B9’ marked ‘Y’.

“Through the use of modern scientific equipments especially the Video Spectral Comparator (VSC 6000), I have discovered different characteristics in strocke formation between the disputed and specimen signatures based on skills, line quality and general appearance.

“Therefore, in my opinion, I here by state that, the disputed signature on exhibit  ‘A’ marked ‘X’ and specimen signatures on exhibits ‘B1 – B7, B8 and B9’ marked ‘Y’ are different and were written by two different persons.”

Na sehemu ya utangulizi wa ripoti hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya taifa na kusainiwa na SP Nestory M. Tagaya kwa niaba ya aliyekuwa Kamishana wa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai ambayo pia Tanzania PANORAMA Blog imeoina, inasomekana hivi; “Pamoja na barua hii, ninakurudishia vielelezo vyote nikiambatanisha na taarifa ya uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na ASP Chrisantus Kitandala aliyechunguza hati hizo,”

Kampuni ya Ravji Construction Ltd inamtuhumu Mkurugezi wa Kampuni MeTL, Murtaza Alihussein Dewji kughushi nyaraka na saini za makubaliano ya kuuziana kiwanja namba 105 na pia kinailalamikia Kampuni ya MeTL kujipatia Dola za Marekani 600,000 zilizoingizwa kwenye akaunti ya MeTL kama malipo ya kiwanja hicho.

Mohamed Dewji, mmoja wa wakurugenzi wa MeTL ambaye alitumiwa maswali yaliyohitaji ufafanuzi kuhusu madai hayo kupitia simu yake ya kiganjani, hadi sasa hajajibu chochote licha maswali kuonyesha kuwa yamepokelewa na kusomwa.

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya