Wednesday, December 25, 2024
spot_img

UTAJIRI ULIOFICHIKA SELOUS LINAPOJENGWA BWANA LA KUZALISHA UMEME LA JULIUS NYERERE

 

RIPOTI MAALUMU (2)

HII ni sehemu ya pili ya ripoti maalumu ya utafiti uliofanywa na watalaamu bingwa wazalendo dhidi ya hekahela za wazungu za kutaka kuzuia mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere katika Mto Rufiji.

Ripoti hii ni matokeo ya fitna za wazungu zilizowainua wataalamu bingwa wa kitanzania wanaotambulika na jumuiya za kimataifa kwa usomi wao kufanya utafiti dhidi ya fitna na uzushi huo uliokuwa na lengo la kukwamisha mradi huo.

Magwiji hao wamefanyia utafiti hoja zote za wazungu zilizolenga kukwamisha jitihada za Serikali ya Tanzania kutekeleza mradi huo na kuandika ripoti ya kina inayojibu upotoshaji wa wazungu.

Ni ripoti iliyofanyiwa utafiti wa kitalaamu kuhusu hofu, majibu ya hofu, athari za mazingira, mipango ya kudhibiti athari za mazingira, faida baki za mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere na unafuu wa gharama za umeme kwa Taifa la Tanzania baada ya mradi huo kuanza kufanya kazi.

Salehe Pamba



SALEH PAMBA, DK. ABUBAKAR RAJABU, *ABDULKARIM SHAH* DK. MAGNUS NGOILE NA DK. THOMAS KASHILILAH

PORI la Akiba la Selous lina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 50,000. Ni moja ya maeneo muhimu zaidi yaliyohifadhiwa barani Afrika na lilitambuliwa kama kituo cha urithi wa dunia tangu 1982.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inalisimamia pori hili kama eneo la viumbehai ambalo liko katika daraja la nne kwa mujibu wa vigezo vya IUCN. Ndani yake kuna makazi ya kudumu ya watu, shughuli za uwindaji unaodhibitiwa na michakato ya utalii.

Bwawa la Stiegler’s Gorge liko katika sehemu ya kaskazini ya hifadhi, na kilomita 180 kutoka Bahari ya Hindi. Korongo la Stigler’s lina urefu wa kilomita nane na kina cha meta 100.

Mro Rufiji



Hifadhi hii ilitambuliwa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1950 wakati wa utafiti wa kwanza wa vyanzo vya maji vya Bonde la Mto Rufiji, ambalo ni kubwa kuliko yote nchini Tanzania.

Uchunguzi wa mwanzo juu ya Stiegler’s Gorge ulifanyika kwa msaada wa wageni, lakini ujenzi wake uliahirishwa mara kadhaa. Badala yake Tanzania iliendeleza mabwawa madogo katika Mto Rufiji na katika maeneo mengine ya nchi.

Maporomoko ya maji yanayoanzia kwenye Korongo la Stigler’s, yaani Mto Rufiji, yanakwenda mpaka kwenye ukanda wenye ardhi nyevu wa Rufiji-Mafia-Kilwa (RUMAKI), ukanda ambao eneo lake ni kilometa za mraba 5,969.

Ukanda huu umeteuliwa na serikali mnamo 2004 chini ya Mkataba wa Ramsar, baada ya Tanzania kuridhia mkataba huo mwaka 2000.

Eneo hili linajumuisha delta nzima ya Rufiji yenye ukubwa wa eneo wa kilometa za mraba zipatazo 1,400 na misitu ya mikoko yenye ukubwa wa eneo wa kilometa za mraba zipatazo 550, maeneo ya pwani kusini mwa delta, kisiwa cha Mafia na maji ya pwani yenye kina kifupi, visiwa na miamba ya matumbawe katikati ya visiwa hivyo.

Msitu wa Mikoko



Hifadhi ya Wanyama ya Selous (SGR) ni makazi ya tembo wa jamii ya Kiafrika, faru mweusi, mbwa mwitu wa jamii ya Kiafrika na idadi kubwa ya viboko na nyati.

Pia kuna idadi ya wanyama muhimu kama vile swala wa jamii ya nyanda za savana, mbwa mwitu wa jamii ya Lichtenstein, swala wa jamii ya kudu, swala wa jamii ya elead na nyumbu wa jamii ya Nyasa.

Mbwa mwitu



Pia, kuna idadi kubwa ya mamba wa jamii ya Mto Nile, pamoja na spishi mbalimbali za ndege kama vile kware jamii ya msitu wa Udzungwa na chozi bawa jekundu.

Mamba



Pia hifadhi ina makazi bora ya viumbe anuwai inayojumuisha misitu ya Miombo, ukanda wa nyasi, misitu inayoambaa kwenye mito na mabwawa.

Sifa hizi zinaifanya hifadhi kuwa kitovu muhimu cha michakato ya kiikolojia na kibaolojia. Hifadhi pia ina msongamano mkubwa wa spishi tofauti zaidi ya 2,100 zinazojumuisha mimea pamoja na wanyama wakiwemo mamalia wengi.

Kwa sababu ya ukubwa wake wa hekta 5,120,000, Pori la Akiba la Selous linayo hulka ya kiikolojia na kibaolojia isiyokumbwa na misukosuko.

Pia linazo hifadhi za spishi anuwai katika makazi tofauti. Pori hili ni sehemu ya ekolojia ya Selous yenye kilometa za mraba 90,000. Ekolojia hii inahusisha mbuga za kitaifa, hifadhi za misitu, barabara za lami ambazo hazina lami, viwanja vya ndege, nyumba za kulala wageni na kambi na jamii ndogo za kudumu.

Bila kujali kama eneo hilo limetengwa kisheria kwa matumizi maalumu au hapana, tunajua kuwa mfumo wa kisheria umeliweka eneo hilo chini ya udhibiti wa haraka wa TAWA, likiwa chini ya uangalizi wa utawala wa mikoa na wilaya kadhaa.

Kwa kuzingatia ukaribu wake mkubwa kuna shughuli kadhaa za kijamii na kiuchumi huko Selous, ambazo ni pamoja na hoteli, nyumba za kulala wageni na kambi za hema, safari za wanyamapori, safari za utalii wa picha, safari za boti, safari za uwindaji, safari za anga, uwepo wa barabara, viwanja vya ndege, wanyamapori, usimamizi pamoja na shughuli za kibinadamu zinazounda uwepo wa binadamu na wanyamapori katika Pori la Akiba la Selous kwa miaka mingi.

Pori la Akiba la Selous pia linaungana na Pori la Akiba la Niassa lililoko nchini Msumbiji.

Pori la Akiba la Niassa, lililo Msumbiji



Pori la Akiba la Niassa lina ukubwa wa eneo wa kilomita za mraba 42,000. Mapori haya mawili yanaunda ukanda mmoja unaounganisha nchi hizo mbili na hivyo kuwa changamoto katika usimamizi wa uhifadhi.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inasimamia asilimia nane ya eneo lililo Kaskazini mwa Pori la Akiba la Selous kwa ajili ya kazi maalumu ya utalii wa picha wakati sehemu kubwa iliyobaki inasimamiwa kama hifadhi ya uwindaji.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya