Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta (katikati mwenye suti nyeusi) Mkuu wa Wilaya wa Arumeru , Jerry Murro,(pembeni ya RC Kimanta) wakikagua ujenzi wa madarasa |
NA MWANDISHI WETU, ARUMERU
MWENENDO wa ufanyaji kazi na utekelezaji wa mipango mikakati ya serikali wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (DC) Jerry Murro umetajwa kuwa wa kumpigia mfano kutokana na mafanikio yanayofkiwa na wilaya yake.
Haya yamethitishwa na matokeo chanya ya usimamizi wake wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika eneo lake la kiutawala, sambamba na kughulikia kero za wananchi pamoja na vita dhidi ya rushwa na wahalifu.
Tayari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Idd Hassan Kimanta amempongeza DC Murro kwa kuutambua mchango wake mzuri kiuongozi wa kusimamia utelekelezaji wa miradi ya serikali katika Wilaya ya Meru.
Katika pongezi zake hizo, RC Kimanta pia alitambua kazi nzuri inayofanywa na uongozi mzima wa Halmshauri ya Meru kusimamia utekelezaji wa mipango mikakati ya serikali ukiwemo ujenzi wa madarasa.
RC Kimanta alitoa pongezi hizo hivi karibuni alipofanyaziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Meru kukagua ujenzi wa madarasa katika halmashauri za Meru na Arusha.
Alisema kasi ya ujenzi wa darasa kama ilivyoelekezwa na serikali katika Halmashauri ya Meru inaridhisha.
RC Kimanta aliutaka uongozi wa halmashauri hiyo kutobweteka na mafanikio hayo bali uongeze nguvu katika kampeni ya ujenzi endelevu wa madarasa inayoratibiwa na DC Muro akisaidiwa na wakurugenzi, wabunge na wenyeviti wa Halmashauri za Meru na Arusha.
Akkzungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya elimu, RC Kimanta alieleza kufurahishwa kwake na jitihada kubwa zilizofanya na kuwezesha ujenzi wa shule tatu mpya alizozitaja kuwa ni Shule ya Msingi Faye Crane Chemchem inayomilikiwa na serikali.
Alizitaja nyingine kuwa ni Shule ya Sekondari ya Elimu Maalumu ya Patandi inayomilikiwa serikali zote pamoja na Shule ya Mchepuo ya Kingereza ya Mringa inamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Alisema anafurahi kuona ujenzi wa shule hizo upo katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza kupokea wanafunzi mapema mwaka huu.
Awali DC Murro katika taarifa yake kwa RC Kimanta kuhusu utekelezaji wa mipango mikakati ya serikali inayolenga kutoa elimu kwa watoto wa taifa zima, alisema katika eneo lake la kiutawala, ifikapo Januari 18, 2021 (leo) madarasa 30 yatakuwa yamekamilika kujengwa.
DC Murro alisema katika mwendelezo huo huo wa utekeezaji wa maagizo ya serikali kuu yanayozitaka serikali za wilaya kujenga madarasa yatayowezesha watoto wote kupata elimu, kabla ya Februari 28 2021, madarasa 28 yatakuwa yamekamilika kujengwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta akionyeshwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru moja ya vyumba vipya vya madarasa vilivyojengwa na serikali ya wilaya ya hiyo |
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo kutafikisha idadi ya madarasa 58 yanayohitajika kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza na hivyo kukamilisha malengo ya serikali yaliyokusudiwa na serikali kuu kutekelezwa na serikali ya wilaya.
DC Jerry Muro anafaa kumrithi Iddi Kimanta. Muro anatakiwa awe mkuu wa mkoa wa Arusha