Wednesday, December 25, 2024
spot_img

BODI YA MIKOPO YAFAFANUA SHERIA YA ULIPAJI MADENI KWA WANAFUIKA WA MKOPO

Mkurugeni Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru

 NA MWANDISHI WETU

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi wa marekebisho ya sheria ya mwaka 2016 ya urejeshaji mikopo kwa wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu unaompa nafasi mnufaika kutumia ujuzi alioupa kurejesha deni lake.

Taarifa ya HESLB iliyotolewa Januari 10, 2021 na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji , Abdul-Razaq Badru, ilieleza kuwa marekebisho ya sheria ya bodi hiyo ya mwaka 2016 yanaelekeza mnufaika ambaye hana ajira kuanza kufanya marejesho 24 baada ya kuhitimu masomo yake.

Badru alieleza katika taarifa yake kuwa muda wa miezi 24 uliongezwa kutoka miezi 12 katika marekebisho ya sheria ya HRSLB ya mwaka 2016 ili kutoa nafasi kwa wanufaika kutumia ujuzi walioupata katika masomo yao kuanza kulipa.

“Baada ya miezi 24 kupita, mnufaika ambaye hajaanza kurejesha atakuwa na tozo ya asilimia 10 juu ya deni lake. Tozo hii hutozwa mara moja tu na inalenga kuwakumbusha wanufaika wajibu wao na kuanza kurejesha ndani ya muda uliowekwa kisheria.

” Sheria ya HESLB inampa mnufaika asiye katika sekta rasmi nafasi ya kurejesha sh 100,000 au asilimia 10 ya kipato anacholipia kodi kwa mwezi. Lengo la utaratibu huu ni kumpa nafasi mnufaika anayetumia ujuzi alioupata chuoni kurejesha au kumaliza deni lake . kwa sasa HESLB ina wanufaika 14,021 waliojiriwa ambao wanarejesha.

“Kufuatia marekebisho ya sheria ya HESLB ya mwaka 2016, mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu anayepata ajira ana wajibu wa kumjulisha mwajiri kuwa ni mnufaika na mwajiri atawasilisha taarifa zake HESLB na tunawasihi wanufaika wote kuwa wazalendo na kujitokeza kuanza kurejesha mikopo kwa wakati ili kuepuka adhabu juu ya Madeni,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo ya Badru inaeleza kuwa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Iddy, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Namonge ya mkoani Geita ikidai kuwepo utofauti wa deni linaloonekana kwenye hati ya mshahara wa mnufaika na taarifa ya deni; ilitokana na uelewa mdogo wa urejesha wa mkopo.

Taarifa ya Badru inaeleza kuwa HESLB iliwasiliana na Mwalimu Idd Jumamosi ya Januari 9, 2021 na kumpa ufafanuzi wa kina kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu na kwamba mwalimu huyo alielewa na kuahidi kuwa balozi mzuri wa bodi.

“Kuhusu utofauti wa deni linaloonekana kwenye hati ya mshahara wa mnufaika na taarifa ya deni, ufafanuzi ni kuwa deni sahihi ni lile lililopo kwenye taarifa ya deni inayotolewa na HESLB  ambalo limezingatia tozo ya kutunza thamani.

” Kwa sasa HESLB Inakamilisha mfumo wa kielektroniki utakaomuwezesha mnufaika kuona deni sahihi kwa njia rahisi ikiwemo simu ya mkononi kuanzia mwezi Februari 2021,” inasomeka taarifa hiyo.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya