Tuesday, December 24, 2024
spot_img

VITA YA KAGERA ALAMA YA UMOJA NA UZALENDO WA MTANZANIA

 

NA GEORGINA ROESER

NIMEMALIZA kuangalia kipindi maalumu cha vita ya Kagera kilichorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC). Ni kipindi chenye matukio mengi ya kujifunza na binafsi kimeniacha najiuliza mambo kadhaa kuhusu Fashisti Nduli Idi Amin.

Nawashauri Watanzania wawe na utamaduni wa kutazama vipindi vya aina hii ili waone matukio halisi yalivyokuwa katika vita hiyo. Ni katika kipindi hicho mtazamaji ataona  wanajeshi wetu waliopigana vita ile walivyopambana. Asanteni sana wanajeshi wetu.

Ninavuta picha joka lile lingeiteka nchi yetu tungekuwa na maisha gani leo. Watanzania wanaosema tulimchokonoza Nduli Idi Amini walishawahi kufikiri hili?

Nimejifunza mengi kwenye kipindi hicho ikiwemo Rais Yoweri Museveni kupigana upande wa majeshi yetu dhid ya joka lile. Na udumu huko Uganda Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Wale mnaompigia kelele ati muda wake umefika atoke hebu kamtizameni huko alivyochezea tope na makombora kibao yakirindima!


Vita ilikuwa na matatizo ya miundo mbinu, sehemu nyingine wanajeshi walibeba silaha nzito kwa sababu magari yalikuwa hayawezi kupita kutokana na mvua iiliyokuwa ikinyesha lakini pia majigambo ya Fashiati Amin yalikuwa yanaumiza sana.

Vita jamani ni majanga. Kama unamfahamu askari yeyote muheshimu sana. Vita ni kitu kibaya  sana. Wananchi walijitolea vyakula, wanyama unawaona wanaswagwa kuchangia vita. Umoja na Uzalendo ule naomba Mungu udumu nchini mwetu. Hivi vipindi TBC waangalie utaratibu na wizara ya Elimu wawaoneshe wanafunzi mashuleni wajue tulipotoka.

Nadhani baadhi yetu huwa tunabeza baadhi ya mambo kwa sababu hatujui historia.

Hamasa zilirembeshwa na:

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

IDUMU SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

ZIDUMU FIKRA SAHIHI

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya